Burudani ya Michezo Live

Kiwanda cha nyama chanzo cha Ongezeko la Corona, Ujerumani 

Kiwanda cha nyama chanzo cha Ongezeko la Corona, Ujerumani 

Kumeshuhudiwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa wakaazi wa mji Gütersloh unaozunguka kiwanda cha machinjio ya wanyama ambacho kilikumbwa na mlipuko mkubwa wa virusi vya Corona.

Hadi sasa maambukizi yalikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa kiwanda cha kusindika nyama cha Tönnies, hata hivyo mripuko huo unaonekana sasa kuanza kusambaa katika jamii.

Ndani ya kipindi cha siku saba, jumla ya kesi 75 zimethibitishwa katika jamii ambayo haina uhusiano na machinjio.

Mji huo unadai kwamba hilo huenda limetokana na ongezeko la upimaji katika eneo hilo.

Wengi wa waliopimwa hawakuonyesha dalili yoyote na hakuna ongezeko la wagonjwa.

Ila kutokana na kuanza kwa likizo za majira ya joto, watu wengi wamepata hamasa ya kupima ili waweze kupata kibali cha kusafiri nje ya maeneo hayo yaliyo chini ya vizuizi.

Hadi kufikia Ijumaa jioni, visa vya mamabukizi vilikuwa ni 2,203 katika mji wa Gütersloh, na wengi wao ni wafanyakazi katika kiwanda cha kusindika nyama au wanahusiana na kiwanda hicho. 748 kati yao wanasemekana kuwa wamepona na waliobaki 1,434 bado wana maambukizi.

Tangu mripuko huo uzuke kwenye mji wa Gütersloh jumla ya watu 21 wamepoteza maisha.

Mripuko huo umesababisha mamlaka za jimbo kutangaza kwamba wafanyakazi wote wa kiwanda cha nyama watalazimika kupimwa virusi vya corona angalau mara mbili kwa wiki kuanzia mwezi Julai.

Makampuni pia yanatakiwa kuorodhesha majina ya watu wote walioko eneo la kiwanda. Wakaazi wa miji ya Gütersloh na Warendorf wamekasirishwa na hatua za hivi karibuni za kufungiwa, Nikolai Galen ni mkaazi wa hapo.Ausbruch von COVID-19 in Gütersloh

“Nadhani haipaswi kuwa na ujumuishaji wa jumla. Kwasababu Gütersloh haimaanishi ni mji mzima wa Gütersloh. Mji ni kubwa na kuna maeneo mengi ambayo yako mbali sana na hayahusiani na hili, lakini yote yameangukia katika vizuizi.”

Wimbi la maambukizi ya COVID-19 nchini Ujerumani linahusishwa kwa kiasi kikubwa na viwanda vya kusindika nyama ambavyo vina mazingiru hafifu ya kufanyia kazi na kuishi kwa wafanyakazi wengi wanaotoka Ulaya mashariki.

Mripuko wa hivi karibuni umechochea kutolewa wito wa kufanyia mageuzi mfumo mzima wa mazingira ya kufanyia kazi katika sekta ya nyama nchini Ujerumani, athari za kiwanda cha Tönnies na miongozo ya kitaifa ya kukabiliana na maeneo yaliyo na mripuko wa virusi vya corona.

Kutokana na mripuko huo, serikali ya jimbo imeamuru kurejeshwa vizuizi katika wilaya ya Gütersloh na Warendorf hadi Jumanne ijayo, pale serikali itakapoamua jinsi gani ya kuendelea.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW