Michezo

Kujilinda si uhalifu – Jose Mourinho

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amekiambia chombo cha habari cha BT Sport kuwa waliutawala vyema mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya hapo jana usiku dhidi ya Benfica huku mlindalango wa timu hiyo, David de Gea akiisaidia kuokoa mipira kadhaa iliyopigwa na wapinzani wao.

Mourinho amesema “Wakati mwingine nafikiri kuamua kujilinda si huhalifu bali ni njia ya kupata matokeo,”amesema kocha huyo.

Jose Mourinho ameongeza kwa kusema “Nilikuwa nafahamu kuwa wapinzani wetu wana golikipa mzuri hivyo niliwataarifu wachezaji wangu mapema hasa kutumia nafasi ya mipira iliyokufa.”

Katika upande mwingine Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amemuambia, Mourinho kuacha kuzungumzia klabu hiyo ya The Blues baada ya bosi huyo wa Old Traford kumuambia Conte analia na tatizo la majeruhi yanayo ikabili timu yake.

Mourinho, ameyasema hayo wakati Chelsea ikitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Roma katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya iliyopigwa hapo jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents