DStv Inogilee!

Licha ya kiwango alichoonyesha Mesut Ozil dhidi ya BATE, Unai Emery asisitiza Mjerumani huyo bado hana nafasi

Mesut Ozil hapo jana amerejea tena kwenye kikosi cha Arsenal baada ya kukosekana kwa muda mrefu ambapo aliweza kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 0 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Europa League.

Licha ya kucheza vema kwenye mechi hiyo kocha mkuu wa Arsenal, Unai Emery amesisitiza kuwa bado nafasi yake ni ndogo ndani ya kikosi chake.

”Leo ameonyesha kile anachohitaji, kama atakuwa yupo tayari kama wiki mbili zilizopita basi tutamshirikisha kwenye mechi nyingi zaidi na hata kuanza kwenye kikosi cha kwanza na hata wakati mwingine akitokea benchi kwakuwa tunawachezaji wengi wanaoweza kutusaidi.”

”Jitihada zake zilikuwa nzuri, ubora, kiwango chake pamoja na ushirikiano wake na wachezaji wengine pia ulikuwa mzuri, nafikiri tunahitaji kila mchezaji kuwa kama hivyo, leo kucheza na Mesut ilikuwa muhimu sana.”

Nyota huyo wa Ujerumani hapo jana amecheza kwenye kiwango kizuri dakika zote 90 mechi dhidi ya BATE ingawaje baada ya mchezo huo Emery amesema kuwa hamuakikishii nafasi ya kudumu Ozil ndani ya timu hiyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW