Tupo Nawe

Lukaku afunguka kibarua cha bosi wake ‘Pasipo na shaka Ole Gunnar Solskjaer atakabidhiwa Man United’

Romelu Lukaku anaamini kuwa pasipo na shaka yoyote, Ole Gunnar Solskjaer atakuwa meneja wa kudumu wa Manchester United baada ya kuiyongoza timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Champions League kwa mara ya kwanza tangu kufanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2014.

Marcus Rashford aliipatia bao la tatu na la ushindi kupitia njia ya mkwaju wa penati baada ya Romelu Lukaku kuiongoza United kwa mabao yake mawili mbele ya Paris Saint-Germain katika dimba la Parc des Princes ugenini.

Kwa matokeo hayo inamaana kuwa United imeshinda mechi 14 kati ya 17 ilizocheza tangu timu hiyo kuwa chini ya kocha Solskjaer akichukua kijiti kutoka kwa Jose Mourinho, wakati ikipoteza mara moja.

Ole Gunnar Solskjaer masterminded Manchester United's stunning comeback win against Paris Saint-Germain

“Nafahamu atasalia hapa, pasina shaka katika hilo kwakuwa anahitaji pia kuendelea kuwa hapa hata wachezaji wanahitaji abakie, tunafanya vizuri sana na tunacheza kama Manchester inavyopaswa kucheza,” Lukaku amekiambia chombo cha habari cha Viasport.

Lukaku ameongeza kuwa “Ni kocha kijana na anawachezaji vijana pia hivyo ni mazingira bora kwa maendeleo na matumaini ya kutwaa taji siku za usoni.”

Lukaku ni miongoni mwa wachezaji waliyocheza wakati United inaibuka na ushindi dhidi ya Tottenham, Chelsea na Arsenal.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW