Bongo5 Makala

Mambo 10 studio zingine za Tanzania zinapaswa kujifunza kutoka MJ Records na B’Hits

Kuongezeka kwa wasanii nchini kunaenda sambamba na ongezeko la studio za kurekodia muziki. Lakini pamoja na kuwepo studio nyingi, ni chache tu zinazofanya vizuri na zinazoheshimika. Sababu kubwa ni ukongwe wa studio hizo, hits zilizotayarisha pamoja, sifa nzuri ya mtayarishaji wake, utawala na mambo mengine.

2222 low
Timu ya B’Hits Kuanzia Kushoto: Deddy, Gosby, Pancho Latino, M-Rap na Dj Choka

Miongoni mwa studio hizo ni pamoja na MJ Records inayomilikuwa na Master Jay lakini producer akiwa Marco Chali na B’Hits inayomilikuwa na Hermy B na producer akiwa Pancho Latino.

Maproducer wengi wa muziki wanaoajiriwa huishia kuhamahama sababu wamiliki wa studio hizo wana kasoro nyingi. Haya ni mambo 10 ambayo studio zingine zinapaswa kuyazingatia.

1. Kumthamini Producer

Master J na Hermy B waliamua kujiweka kando kiasi na kuleta maproducer wengine kusimamia studio hizo. Master Jay alimchukua Marco Chali kutoka Kama Kawa Records takriban miaka 7 iliyopita, huku Hermy B akimtoa Pancho Latino kutoka Dhahabu Records na hadi leo maproducer hao si tu hawajawahi kuondoka, bali hawana kabisa mpango wa kuondoka. Sababu kubwa ni namna wanavyothamiwa.

2. Uhuru kwa Producer

Ukiwa mmiliki wa studio na ukataka kumsimamia producer kwa kila anachokifanya na ukahisi anaweza kupiga vimeo, ni rahisi kuanza kuonekana bosi mkuda na kumnyima producer uhuru. Marco Chali na Pancho Latino wana uhuru mkubwa katika studio hizo, imradi tu hawavunji sheria za kawaida. Ndio maana Marco Chali amekuwa na uhuru hadi wa kuanzisha Marco Chali Foundation ambayo inapewa support na Zantel. Master Jay angekuwa mswahili, angeleta zengwe kwa fikra kuwa Marco anafaidi sana.

994909_10201826866457456_214687561_n
Marco Chali akiwa na mdogo wake Frank Chali aka BeefCha. Beefcha ameproduce ngoma kadhaa ikiwemo ya Micharazo BOB Wamekaa,HipHop ya Slim Sal na zingine.

3. Mchukulie Producer kama partner na sio kama Mwajiriwa

Marco Chali na Pancho Latino katika studio zao hawachukuliwi kama waajiriwa, bali ni kama partners. Hisia hiyo huwafanya wafanye kazi kwa kutofikiria malipo bali hufikiria kufanya kazi kwa bidii kuzipeleka mbele zaidi studio zao.

4. House Style/Identity

B’Hits ni mabingwa wa hili. Hawa jamaa wana namna yao peke yao ya kufanya kazi na huenda hawafanani kabisa na studio zingine. Ni jambo zuri kila studio ikiwa na utambulisho wao na namna yake ya kufanya kazi.

5. Professionalism

MJ Records na B’Hits zimetoka kwenye kuwa kama studio tu bali pia kama kampuni. Na ndio maana B’Hits ni Music Group ikiwa na matawi Tanzania na Kenya. Kazi zao wanazifanya kama ofisi kubwa zifanyazo mathalan mikataba ya wasanii na mambo mengine. Kukaa Marekani kwa Hermy kumemfanya ajifunze jinsi studio za huko zinavyofanya kazi na amekuwa akijaribu ku’apply’ baadhi ya mambo yanayowezekana kwa Tanzania kwenye studio yake.

6. Utaratibu wa kuachia nyimbo

Sitotaja jina, lakini kuna producer wa studio moja ambaye kila siku huwa napata email mbili ama tatu za nyimbo mpya. Utawezaje kuachia nyimbo tatu kila siku? Zinaenda wapi? MJ Records na B’Hits wanaweza wakae hata miezi 6 bila kuachia nyimbo na hiyo haimaanishi kuwa hakuna nyimbo wanazorekodi. Ni utaratibu tu waliojiwekea katika kuachia nyimbo na sio ‘bora nyimbo’. Quality ni bora kuliko Quantity.

7. Hakuna ubosi

Marco Chali anamchukulia Master J kama ‘bro’ na Pancho kwa Hermy hivyo hivyo. Hakuna ubosi ndio wamedumu.

Pancho
Pancho Latino, producer wa B’Hits

8. Ubahili ni adui

Kama producer anaingiza fedha nzuri, kwanini mmiliki usimlipe vizuri na kumfanya afurahi? B’Hits na MJ Records wanaujua mchezo.

9. Ushirikiano

B’Hits ni mfano mzuri katika hili. Wimbo mmoja unaweza kushambuliwa na watu zaidi ya wanne. Pancho atatengeneza mdundo, msanii ataingiza sauti, Hermy B atakuja kufanya mastering ama kuutuma Kenya kwa Randy wa B’Hits Kenya kuongeza kitu pia. Wimbo ukitoka unakuwa na ubora unaotakiwa. Kwa upande wa MJ Records tunafahamu jinsi Marco Chali anavyowatumia wadogo zake kutengeneza ladha tofauti za midundo.

10. Hakuna Ubabaishaji

Hii ni sababu kwanini MJ Records inaongoza kwa kutengeneza matangazo mengi ya biashara. Makampuni makubwa kama ya simu hutumia advertising agency zinazoendeshwa kisomi. Haziwezi kufanya kazi na studio zenye longo longo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents