DStv Inogilee!

Manara amvisha jezi ya Simba Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ambaye amewahi kuwa msemaji wa Yanga

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameamua kumvisha jezi ya timu hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro wakati mabingwa hao watetezi wakiwa Arusha kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid kuikabili African Lyon mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Julai 14 mwaka 2017 klabu ya Yanga kupitia kwa aliyekuwa katibu wake Mkuu kwa wakati huo, Charles Boniface Mkwasa ilimtambulisha, Jerry Muro kuwa msemaji wa timu hiyo na kutikisa sana katika nyanja ya kimichezo hasa kufuatia ushindani wake dhidi ya Haji Manara ambaye anatokea upande wa hasimu wao Simba SC.

Licha ya Jerry kuwa Mkuu wa Wilaya lakini ushawishi wake kwenye soka la Tanzania bado upo mkubwa hasa ukizungumzia klabu hizi mbili za kubwa za watani wa jadi Simba na Yanga.

Wiki iliyopita Yanga imejikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya Simba baada ya kufungwa bao 1 – 0 kwenye mechi ya ligi kuu soka Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW