Diamond Platnumz

Mashavu ya show yanazidi kumdondokea Diamond Platnumz! Yeye na Mr Flavour kushiriki kampeni ya Coca Cola nchini Kenya (July), na baadaye kufanya show nyingine Nairobi na Mombasa (August)

Huu ni mwaka wa Diamond Platnumz ‘sukari ya warembo’ kubadilisha kabisa maisha yake kutokana na mashavu ya show zinazoendelea kumiminika kwa wingi na kwa kufuatana. Ni jana tu mwenzangu Fred Bundala ameandika juu ya makadirio ya kile tunachohisi Platnumz atakuwa ameweka katika akaunti yake ya benki kwa show za mwezi huu (June/July) peke yake. Lakini tumepata taarifa juu ya show zingine anazotegemewa kufanya mwezi wa 8 nchini Kenya.

Diamond6

Mtandao wa Standard Digital Entertainment umethibitisha kuwa staa huyo wa hit ya ‘Kesho’ anategemea kufanya show nyingine katika viwanja vya Carnivore (August 9) jijini Nairobi, na kesho yake (August 10) ataelekea Mombasa katika show nyingine itakayofanyika katika hoteli ya Whitesands, hizi zote zikiwa zimeandaliwa na The Courtyards.

Pia jana tuliripoti juu ya show anayotegemewa kutumbuiza jukwaa moja na wasanii wa kimataifa kutoka Nigeria Ice Prince na Davido itakayofanyika Nairobi (July 27).

Ukiachilia show hizo Platnumz akiwa kama Coca boy anategemewa kushiriki katika kampeni ya Coca cola kama tunavyojua yeye ni balozi , ambapo akishirikiana na Mr Falvour wa Nigeria wataurudia nyimbo za marehemu Brenda Fassie “Vulindlela” pamoja na ule wa 2 Face Idibia “African Queen”.

Hivi ndivyo muziki unaweza kubadilisha maisha ya kijana wa kiTanzania endapo utauchukulia serious kama kazi, juhudi na uvumilivu ndio silaha ya vita hii. Big up Platnumz you deserve it man.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents