Uncategorized

Mechi tatu tu, Ole Gunnar Solskjaer avunja rekodi Manchester United nakuweka yakwake

Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa kocha wa kwanza katika historia ya klabu hiyo kuweza kuibuka na pointi tisa na mabao 12 kwenye michezo yake mitatu ya kwanza toka kuanza kibarua chake.

Image result for Twelve goals and nine points sees the interim boss make the best ever start in the opening three games of any manager in the club's history

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya michezo barani Ulaya, Ole Gunnar Solskjaer ameweka rekodi hiyo baada ya kuwa kocha wa kwanza ndani ya historia ya Manchester United kwakuwa na idadi hiyo kubwa ya mabao kwenye mechi tatu nakujizoelea pointi zote tisa kwa michezo yake ya kwanza toka kukabidhiwa timu.

Paul Pogba, Marcus Rashford, Romelu Lukaku wakiiwezesha timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 4 – 1 dhidi ya Bournemouth.

Aliyewahi kuweka rekodi ya namna hiyo kwenye klabu ya Manchester United ni kocha, Sir Matt Busby na Jose Mourinho wakishinda michezo yao mitatu ya kwanza walipoanzaajira zao lakini wakizidiwa kiwango cha mabao.

Akizungumzana Sky Sports kiungo wa timu hiyo, Paul Pogba amesema kuwa wanaendelea kushinda kwasababu kocha wao anafundisha kwa staili ya kipekee.

“Tunajivunia, tunatengeneza nafasi nyingi na kuwa kwenye kiwango cha juu, kocha anatutaka tushambulie na hicho ndicho tunachokifanya kwenye uwanja.’’

Chini ya Solskjaer United imecheza michezo yake mitatu dhidi ya Cardiff City, Huddersfiel na Bournemouth na kujivunia mabao 12 na pointi tisa.

Manchester chini ya kocha Busby, ilifanikiwa kushinda michezo mitatu ya mwanzo wakati alipoanza kuifundisha na kuvuna mabao nane, wakati wa zama za Jose Mourinho alishinda mechi zake tatu za mwanzo alipokabiziwa timu na kupata magoli sita pekee ambapo ni tofauti na Solskjaer akifanikiwa kupata jumlaya mabao 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents