Uncategorized

Michael Wambura mikononi mwa TAKUKURU, atangaza kuachana na shughuli zote za soka

Aliyekuwa Makamu wa rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Michael Wambura ametangaza kuachana na shughuli zote za kuongoza mchezo huo.

Mwezi Aprili mwaka jana, Wambura alifungiwa na kamati ya maadili ya TFF, kutojihusisha na maswala ya soka maisha kwa makosa matatu kwa mujibu wa kamati hiyo ambayo ni kupokea/ kuchukua fedha za TFF za malipo ambayo haya kuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanuni za maadili TFF toleo la mwaka 2013.

Jingine ikiwa ni kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya kampuni ya Jeck System Limited ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha kanuni za maadili za TFF toleo la 2013. Hata hivyo kupitia kwa wakili wake Ebenezer alikata rufaa.

Hivi karibuni, Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilitangaza kumfungia Wambura maisha kujihusisha na soka.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kumshikilia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Michael Wambura (pichani) kwa tuhuma za rushwa na leo itamfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. .

Wakati huohuo Wambura kupitia kwa wakili wake Emmanuel Muga ametangaza rasmi kuachana na masuala ya soka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents