Uncategorized

Mkuu wa kampeni za Trump afungwa kwa udanganyifu, kodi yamponza

Meneja wa zamani wa kampeni za rais wa Marekani Donald Trump Paul Manafort amehukumiwa kifungo cha miezi 47 jela kwa udanganyifu katika ulipaji wa kodi na benki.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuficha mamilioni ya dola wakati alipokuwa balozi nchini Ukraine.

Anatarajiwa kuhukumiwa katika kesi nyingine wiki ijayo kwa kufanya kampeni kinyume cha sheria.

Mashitaka hayo yalitokana na na uchunguzi uliofanyika juu ya ikiwa maafisa wa kampeni ya Trump walifanya njama na Urusi ili kumuwezesha apate ushindi katika uchaguzi wa 2016.

Balozi maalumu wa wizara ya sheria ya Marekani Robert Mueller anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake wa miezi 22 ambao unalenga urais wa Trump.

Mchoro wa mahakamani wa Paul Manafort

Nini kilichotokea wakati wa kusikilizwa kwa kesi?

Manafort – ambaye aliaminiwa kwa kazi yake – atalazimika pia kulipa marejesho ya dola milioni $24 pamoja na faini ya dola $50,000.

Manafort mwenye umri wa miaka 69-aliiambia mahakama Alhamisi jioni katika mji wa Alexandria, Virginia, kwamba ” miaka miwili iliyopita imekuwa migumu sana katika maisha yangu “.

” Kusema nimeaibishwa na kudhalilishwa haitoshi ,” aliongeza , huku akimtaka jaji “amuhurumie”.

Aliyaelezea maisha yake kama maisha yaliyogubikwa na “mkanganyiko wa kitaaluma na kifedha” ?

JajiTS Ellis alisema kuwa alishangazwa na kwamba Manafort “hakuonyesha majuhto kwa kujihusisha na mienendo isiyo sahihihi “.

Hata hivyo alisema kwamba hukumu iliyopendekezwa na upande wa mashtaka iliyomuombea kifungo cha miaka kati ya 19.5 na 24 gerezaji ilikuwa ni “kubwa kupita kiasi”.

hukumu yake ni ishara ya kushuka kwa hadhi ya afisa huyo maarufu wa kisiasa wa ngazi ya juu wa chama cha Republicanambaye alikuwa mshauri wa marais wanne wa Marekani akiwemo rais Trump,na viongozi wa kigeni.

Manafort aliyepigwa picha na Donald Trump
Image captionManafort aliyepigwa picha na Donald Trump katika kikao cha Republican mjini Cleveland, Ohio,mwezi Julai 2016

Waendesha mashtaka wanasema Manafort alishindwa kulipa kodi ya zaidi dola milioni sita $6mwakati akiishi maisha ya anasa ikiwa ni pamoja na kununua $15,000 koti lililotengenezwa kwa ngozi ya mbuni na ukarabati wa jumba lake la kifahari la Hamptons.Trump aonywa asivuruge uchunguzi wa Mueller

Manafort alikuwa wenyekiti wa kampeni za Trump kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Juni hadi Agosti 2016, kabla ya kulazimishwa kujiuzulu ili achunguwe kwa kazi yake nchini Ukraine.

Alikuwa ni mshirika wa karibu wa Bwana Trump kukamatwa katika uchunguzi wa jopo maalum , mwezi Oktoba 2017.

Picha ya jela ya Paul Manafort
Image captionManafort atafungwa katika gereza la kitaifa la Cumberland, Maryland

Katika hatua ambayo haikutarajiwa mwezi Februari, mawakili wa Manafort walifichua mahakamani kwamba mteja wao alimshirikisha Bwana Kilimnik ndata za kampeni za uhaguzi za Trump za mwaka za 2016.

Wakosioaji wa rais pia wanasema kuwa Manafort alikuwepo katika jengo Trump Tower June 2016 kwa mkutanobaina ya wafanyakazi wa kampeni na wakili mwenye uhusiano na utawala wa Urusi ambapo aliahidi kufanya kile alichokiita “uchafu” dhidi ya mgombea wa Democratic wakati huo Hillary Clinton.

Robert Mueller
Image captionJopo maalum linatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa mwanasheria mkuu wa Marekani

Nini kinaendelea kuhusu uchunguzi wa Mueller?

Jopo maalumu linatarajiwa kuwasilisha ripoti yake hivi karibuni kwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr.

Wanasiasa wanashauku kubwa ya kupata matokeo juu ya ikiwa kampeni ya Trump ilifanya njama na Urusi au ikiwa Bwana Trump hakufuata sheria katika kuvuruga uchunguzi huo.

Rais Trump amekwishakana kushirikiana na kuvuruga uchunguzi na urusi imekanusha kuingilia uchaguzi wa Marekani.Trump ”alitaka FBI kusitisha uchunguzi wa Flynn”

Washirika wengine watano wa Trump wamekwishashtakiwa kutokana na uchunguzi wa Bwana Mueller.

kamailivyo kwa Manafort, hakuna hata mmoja wao aliyeshitakiwa kwa uhalifu wa kushiriki katika njama za kuvuruga uchaguzi wa 2016 .

Afisa wa zamani wa kampeni Riff Rick Gates na George Papadopoulos, mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani Michael Flynn na wakili binafsi wa Trump Michael Cohen wote kwa pamoja walikiri makosa dhidi yao.

Mshauri wa muda mrefu wa Trump Roger Stone alikana mashtaka dhidi yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents