Habari

Mwimbaji Lauryn Hill atoka jela baada ya kutumikia kifungo cha miezi 3

Mwimbaji, rapper, producer na muigizaji Lauryn Hill kutoka Marekani ameachiliwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Lauryn hill

Laurin Hill (38) ambaye alifahamika zaidi kupitia kundi la Fugees ametoka jela jana Ijumaa (October 4) lakini atakuwa kwenye probation ya mwaka mmoja ikiwa inajumuisha miezi mitatu ya kifungo cha nyumbani.

Kwa mujibu wa Washington Post, wakili wake amesema Hill aliyehukumiwa kwenda jela mwezi (July) ameachiliwa huru siku chache kabla ya kifungo kuisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na tabia nzuri aliyoionesha.

Hill, ambaye alianza kuimba na kundi la Fugees katika miaka ya (1990) kabla ya kutoa album yake ya solo “Miseducation” mwaka (1998), alikutwa na hatia mwaka jana kwa kushindwa kulipa kodi ya zaidi ya $ 1,800,000 alizozichuma kuanzia mwaka (2005) hadi (2007).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents