Uncategorized

‘Nawashtaki wazazi wangu kwa kunizaa’- Raphael Samuel

Bwana mmoja mwenye miaka 27 nchini India anapanga kuwashtaki wazazi wake kwa kumzaa bila ridhaa yake.

Bwana huyo aitwae Raphael Samuel ambae ni mfanyabiashara ameiambia BBC ya kuwa si sahihi kuzaa watoto kwa sababu watapambana na magumu ya maisha katika umri wao wote watakaoishi duniani.

Bw Samuel, yumkini anafahamu kuwa ridhaa haiwezi ombwa kabla ya kuzaliwa, lakini anasisitiza kuwa, “hayakuwa maamuzi yetu kuzaliwa”.

“Hivyo, hatukuomba kuzaliwa. Inabidi tulipwe kwa maisha yetu yote ili tuishi,”

Madai kama haya yanaweza kuzua mgogoro kwenye familia yeyote ile, lakini Bw Samuel ana mahusiano mazuri na wazazi wake, ambao wote wawili ni wanasheria, na wanalichukua suala hilo kama kichekesho.

Bi Kavita Karnad ambaye ni mama mzazi wa bwana huyo imebidi atoe tamko kutokana na “kadhia aliyoianzisha mwanangu hivi karibuni.”

“Kwanza, navutiwa kwa ujasiri aliouonesha mwanangu kwa kutaka kutupeleka mahakamani akijua fika kuwa sisi ni wanasheria. Na iwapo Raphael atatupa maelezo yenye mashiko juu ya namna gani tungepata idhini yake kabla hajazaliwa, basi nitakubali makosa yangu,” amesema mama huyo kwenye taarifa yake.

Imani hiyo ya Bw Samuel inatokana na filosofia anaoifuata ijulikanayo kama anti-natalism – ambayo inafundisha kuwa maisha yamejaa shida tupu na hivyo watu waache kuzaana mara moja.

Hilo likiwezekana, basi taratibu binadamu wataondoka kwenye uso wa dunia halia mabayo itaikoa sayari hii.

“Hakuna haja ya kuwa na binaadamu. Watu wengi wanateseka na shida za dunia. Iwapo wataisha, dunia na wanyama watakuwa ni wenye furaha kabisa, maana watastawi. Pia hakutakuwa na binaadamu watakaoumia kwa shida na madhila. Maisha ya binaadamu hayana maana kabisa.”

Mwaka mmoja uliopita, alianzisha ukurasa wa Facebook uitwao Nihilanand, amabao una picha kadhaa akiwa na ndevu ndefu za bandia na mabango tele ya ujumbe wa filosofia yake.

“Kulazimisha mtoto azaliwe na kumlazimisha awe na kazi ni sawa na kumteka na utumwa tu?” ni moja ya mabango yake na pia, “Wazazi wako walikuzaa wewe badala ya kunua mwanasesere ama kufuga mbwa. Hawakudai chochote, wewe ni starehe yao tu .

Raphael ana sema alianza kuwa a fikra hizo toka akiwa na umri wa miaka mitano.

“Nilikuwa mtoto wa kawaida kabisa. Siku moja nilikuwa na hasira na sikutaka kwenda shule, lakini wazazi wangu walinilazimisha kwenda. Hivyo nikawauliza: ‘Kwa nini mlinizaa? Baba yangu hakuwa na jibu. Naamini laiti angelinijibu siku ile labda nisingeendelea kuwaza hivi.”

Jinsi mawazo hayo yalivyoendelea kukuwa akaamuwa kuwaeleza wazazi wake. Anasema mama yake aliyapokea “vyema” lakini baba yake bado “anajifikiria” juu ya wazo hilo.

“Mama amesema alitamani kuonana na mimi kabla ya kuzaliwa kwangu, na laiti angelifanikiwa basi nisingezaliwa,” anasema Raphael huku akicheka na kudai kuwa naona hoja kwenye jibu la Mama yake.

“Ameniambia kuwa alikuwa bado yu mdogo kipindi ananizaa na hakujua kama alikuwa na chaguo lengine, Lakini hiyo ndiyo hoja yangu, kila mtu ana chaguo la kufanya katika maisha yake.”

Katika taarifa yake, mama wa bwana huyo amesema si busara kulichukulia kwa wepesi jambo ambalo mwanawe analiamini.

“Imani yake juu ya mzigo dunia inaobebeshwa kutokana na rasilimali zake kutokana na maisha ya watu, machungu yake juu ya watoto ambao wanakumbana na shida chungu tele wakiwa wanakuwa na madhila mengi yamesahaulika kabisa.”M

“Nina furaha kubwa kuona mwanangu amekuwa mtu ambaye hana woga, na yupo huru katika fikra zake. Yupo kwenye njia sahihi ya kufikia furaha maishani mwake.”

Raphael anasema anaenda mahakamani kwa sababu moja tu kuwa dunia itakuwa sehemu salama zaidi bila ya uwepo wa wanaadamu na si inginevyo.

Miezi sita iliyopita wakiwa wanapata kifungua kinywa, alimwambia mama yake kuwa anajipanga kumpandisha kizimbani.

“Amesema hana neno, lakini amenionya kuwa nisifikirie kuwa atanionea huruma mahakamani. Ameniambia ataniangamiza mahakamani. “

Kwasasa bwana huyo anatafuta wakili, lakini inamuwia vigumu.



Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents