Uncategorized

Ole Gunnar Solskjaer akiri United inahitaji miaka kadhaa ili kuwa na uwezo wa kutwaa kombe la ligi kuu Uingereza

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametilia shaka uwezekano wa klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu msimu huu.

Lakini ameongeza kuwa hakuna haja ya kufanya marekebisho ya kikosi chake ili kushinda taji hilo.

United wameshinda mechi tisa kati ya 10 tangu Solskjaer alipochukua nafasi ya Jose Mourinho aliyefutwa kazi mwezi Desemba mwaka jana.

Manchester United wanashikilia nafasi ya tano katika msimao wa ligi wakiwa nyuma ya mahasimu wao Liverpool na Manchester City kwa alama 14.

“Mwaka huu tuko mbali kidigo, bila shaka,”amesema Solskjaer mbele ya vyombo vya habari.

“Inabidi tukimbizane na timu zilizo mbele yetu, hususan City, Liverpool na Tottenham ambao wanaonekana kuwa wameimarika kimchezo.”

“Tunahitaji miaka miwili mpaka kuweza kuchuku kombe hili. Miaka miwili’ sio muda mrefu, lakini pia sio muda mfupi wa kusema tunaweza kuonesha tofauti mkubwa katika maandalizi yetu, na kila kitu.”

Raia huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 45 ambaye alishinda tuzo ya meneja wa mwezi wa ligi ya Uingereza mwezi Januari tayari ana ”taswira” ya jinsi “Hii timu ya Manchester United itakavyo kuwa katika kipinda cha miaka michache”, hata kama hatapewa kazi ya kudumu.

Alipoulizwa klabu hiyo inahitaji wachezaji wangapi ili kushinda taji hilo, Solskjaer alisema: “inategemea pia utendakazi wa wachezaji waliopo kwa sasa.

“Ikiwa kila mchezaji anaweza kuboresha mchezo wake kwa kati ya 1-2% na wala sio idadi ya wachezaji.

“Kununua wachezaji nyota pekee haitoshi, tulibadilisha mambo mawili matatu na ghafla tumefikia nafasi ambayo ni rahisi kushinda taji.”

Mchezaji huyo wa zamani wa United, ambaye leo atashuka uwanjani kucheza na Fulham anaamini watakuwa tayari kuwania kombe hilo mwaka ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents