Siasa

Rais Kikwete atoa tamko la Mabomu

mjeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea eneo la Jeshi liliopo Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na kusisitiza muda wa hatari umekwisha pita na kuwasihi Watanzania hasa wale walioathirika warudi manyumbani kwao, na wawe watulivu kwani hali ya usalama upo kwa sasa.

 

Msemo huo ulifuatia mlipuko wa mabomu yaliyotokea katika ghala la jeshi huko Ukonga na kusababisha milipuko na baadaye mchafuko wa amani kwa wananchi waliokuwa katika eneo lililo karibu na maeneo hayo.

Wananchi wengi walionekana kuyaacha makazi yao pamoja na biashara zao na kukimbia ili kujisalimisha maisha yao. Wengi walijikuta wakijeruhiwa na hata kupoteza maisha yao kwa kugongwa na magari kwa hali ya vurugu iliyokuwa imejitokeza.

Hali imekuwa tete kwenye maeneo ya Ukonga, Tabata, na hata uwanja wa ndege kwani bado wananchi wengi wanaonekana kutoridhika na hali ya usalama na kukataa kurudi katika makazi yao.

Wananchi wengi wakiwemo watoto wameweka kambi katika uwanja wa Uhuru baada ya kupotezana na wanafamilia wenzao pamoja na kupoteza makazi kwasababu ya milipuko.

 Majeruhi wengi walionekana katika hospitali ya Amana iliyopo Ilala pamoja na Hospitali kuu ya Muhimbili. Wananchi wengi wamehamasika na kuenda kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kuchangia damu hospitalini pamoja na misaada kama chakula na mavazi kupitia taasisi mbalimbali za misaada ikiwemo ile ya msalaba mwekundu.

Inasemekana mpaka sasa wananchi zaidi ya 40 wamepoteza maisha yao na wengine mia moja wakiwa wameumia na kuhitaji matibabu

Tuwaombee uzima Watanzania wenzetu.

Mungu Ibariki Tanzani

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents