Habari

Rais Magufuli kutawanya bilioni 200 Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa kuanzia mwezi ujao atatawanya shilingi bilioni 200 kwajili ya kulipa madeni ya ndani yakiwepo madeni ya walimu.

Akiongea leo baada ya kukutana na Gavana mpya wa Benki Kuu (BOT), Profesa Florens Luoga na Gavana wa BOT anayemaliza muda wake Profesa Benno Ikulu jijini Dar es salaam.

“Kwasababu sasa hivi uchumi unaenda vizuri angalau Kuanzia mwezi ujao wapo watu wanaotudai, wapo masupply waliosupply vyakula kwenye vyuo kwenye mashule, wapo macostrator na wapo wafanyakazi wenye madeni kama walimu, yale madeni ya ndani yale yote yaliyokuwa yamehakikiwa nitaanza kulipa mwezi ujao, nitatawanya bilioni 200 ili ziweze kulipa madeni hayo ningeweza kutoa kesho au kesho kutwa nimeona tuhakiki kwanza,” amesema Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents