Uncategorized

Slovenia: Mbunge ajiuzulu baada ya kuiba mkate dukani, spika adai ni kitendo kisichokubalika

Mbunge mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu ”sandwich” katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia.


Mkate maarufu aina ya sandwich

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo na walikua wakiendelea na shuguli zao.

Hakujulakana kama ameiba lakini baadae baadhi ya wanachama walisisitiza arudi kulipa pesa ya mkate huo.

Krajcic

Krajcic ameomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya.

Suala lake la kuiba lilisambaa baada ya kuwaambia wabunge wengine wakati wa mkutano wa kamati siku ya Jumatano.

”Nilisimama pale kwa dakika tatu, kabla ya kunihudumia,” mbunge huyo mwenye miaka 54 alisimulia katika kituo cha runinga cha mtu binafsi.

Wafanyakazi watatu wa duka hilo hawakugundua kama yupo baada ya kuwa walikua na mazungumzo baina yao hali iliyosabisha profesa huyo wa zamani kujaribu bahati yake.

”Hakuna mtu yoyote aliyepiga kelele, wala kunifuata.”Wabunge wenzake walicheka baada ya kusikia kisa hicho.

Lakini siku ya Alhamisi spika wa bunge hilo Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.

”Amechukua hatua za kuwajibika na kujiuzulu yeye mwenyewe,” Golubovic aliviambia vyombo vya habari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents