Soggy Doggy awa mkurugenzi wa vipindi Ebony FM Iringa
Rapper mkongwe na mtangazaji wa radio nchini, Anselm Ngaiza aka Soggy Doggy amehamia kituo cha radio cha Ebony FM kilichopo mkoani Iringa.
Soggy amehamia kwenye kituo hicho akitokea Uhuru FM na kupewa cheo cha mkurugenzi wa vipindi, Program Director.
“Masikio yako ndio yatafanya ujue upi ni muziki mzuri na upi mbaya….Trust me-Somewhere in Iringa,Tanzania,” aliandika kupitia Facebook. Soggy pia amewahi kuwa mtangazaji wa Triple A FM ya Arusha na Radio Free Africa ya Mwanza.