Uncategorized

Solskjaer amuweka sayari moja Marcus Rashford na nyota hawa hatari duniani, ni baada ya kutimiza michezo 150

Muda mchache baada ya kushinda mechi yake ya saba na kuzidi kujiwekea rekodi akiwa meneja mpya ndani ya klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amwagia sifa nyota wake Marcus Rashford.   

Marcus Rashford continued his fine run of form for Manchester United on Saturday afternoon

Solskjaer amesema kuwa kiwango anachokionyesha Rashford ni kipimo tosha cha nyota huyo kujiamini na kumlinganisha kipaji chake na lejendi Wayne Rooney na mchezaji bora kabisa duniani Cristiano Ronaldo.

‘’Kama utaangalia mwanzo wake, niliwaambia kwamba ni mchezaji mdogo zaidi ya Ronaldo na Rooney kufikisha jumla ya michezo 150 akiwa ndani ya Manchester United,’’ amesema Solskjaer.

Rashford scored as United beat Brighton & Hove Albion in the Premier League at Old Trafford

‘’Sio mbaya, amefikisha michezo 150 akiwa na umri wa miaka 21, lakini pia uwezo wake umekuwa mkubwa na amekuwa mzuri kwenye safu ya umaliziaji na ni ndoto zangu kuwa na mchezaji kama yeye kwenye timu,’’

Interim manager Ole Gunnar Solskjaer, pictured watching from the dugout, was impressed

 Alipoulizwa kama Rashford anaweza kumuweka kwenye kariba ya Rooney na Ronaldo walivyokuwa United wakati wa zama hizo bila kusita Solkjaer alisema ndiyo anamuweka kwenye levo hizo za juu kabisa.

United's red-hot No 10 has now scored five goals in six Premier League games under Solskjaer

Solskjaer ameshuhudia mshambuliaji huyo kinda wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 akitupia bao lake la pili wiki iliyopita huku likiwa lasaba kwenye mechi zake 10 zilizopita.

Solkjaer ameongeza kuwa ‘’Unapokuwa naye kwenye mazoezi uwanjani, huzungumza naye mambo mengi ili kufahamu kilichopo kichwani mwake,’’

‘’Alikuwa anakosa nafasi kabla sijaja lakini nilipofika nilizungumza naye na kumuambia hakuna tatizo juu ya hilo,’’ Meneja huyo wa United anaonekana kuvutiwa mno na kipaji cha Rashford.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents