Uncategorized

Son Heung-min, aridhia ombi la baba yake, atakiwa kutokuoa mpaka atakapostaafu soka

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Korea Kusini, Son Heung-min amekubali maombi ya baba yake mzazi yanayomtaka asioe mke mpaka pale atakapo staafu soka.

Son ambaye anamtazama mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Ronaldo kama role model wake amekuwa na mafanikio mazuri na kuwa chaguo la kwanza la kocha Mauricio Pochettino.

Mkorea huyo amesema kuwa baba yake siku zote amekuwa akitamani kumuona akifanikiwa, ilifikia wakati hadi kuadhibiwa yeye na kaka yake kwa kupiga dana dana pale wanapopigana.

Staa huyo wa Tottenham amekiambia chombo cha habari cha Guardia, “Hutupatia saa nne za kupiga dana dana sote, ndani ya saa tatu tu naona mipira mitatu mitatu machoni mwangu na ardhi yote nyekundu, nikiwa nimechoka na yeye hukasirika,” amesema Son.

Son Heung-min ameongeza “Wakati nilipokuwa na umri wa miaka 10 au 12 na kuja kwa kocha wangu wa timu ya shule na kufanya naye mazoezi tukiwa wachezaji 15 hadi 20. Akiwa na program kwa sisi sote ya kuwa na mpira kwa dakika 40.

“Wakati mmoja kati yetu akiangusha mpira baba yangu hasemi kitu lakini ninapoangusha mimi wote tunaanza upya kupiga dana dana.”

“Cristiano Ronaldo ni role model wangu, anafanya kazi na kujituma zaidi ya kipaji alichonacho. Nimeona wachezaji wengi ambao hawana utimamu wa mwili ambao wanadhani kipaji pekee kinatosha bila juhudi kitu ambacho siyo kweli.”

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 huku amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 14 katika michezo 23 aliyocheza mwaka amekiri kukubaliana baba yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents