Uncategorized

Sudan: Upinzani waombwa kumchagua Waziri Mkuu

Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji.

Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua.

Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita.

Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia

Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum.

Je baraza la kijeshi limesema nini?

Katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili, msemaji Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto ameeleza kwamba baraza la kijeshi lipo “tayari kuidhinisha” serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani.

“Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua,” alisema akimaanisha upinzani na makundi yanayoandamana.

Ameeleza pia kwamba jeshi halitowaondoa waaandamanaji kwa lazima lakini ametoa wito kwa waandamanaji hao “kuruhusu maisha yaendelee kama kawaida” na waache kuweka vizuzi kinyume cha sheria.

“Kushika silaha hakutoruhusiwa,” aliongeza

Baraza la kijeshi pia limetangaza baadhi ya maamuzi yakiwemo:Viongozi wapya wa jeshi na polisi.

Mkuu mpya wa kitengo cha ujasusi (NISS)

Kamati za kupambana na rushwa na kuchunguza chama tawala kilichoondoka

Kuondolewa kwa marufuku zote na kubanwa kwa vyombo vya habari

Kuachiwa kwa maafisa wa polisi na jeshi waliozuiwa kwa kuungamkono waandamanaji.

Ukaguzi wa wajumbe wa kidiplomasia, na hatua ya kutimuliwa kwa balozi wa Sudan nchini marekani na Uswizi.

Demonstrators in Khartoum paint a mural reading "Freedom", 14 April 2019

Kitu gani kimekuwa kilifanyika Sudan?

Maandamano ya kupinga kupanda gharama ya maisha yalianza Desemba mwaka jana lakini punde tu yakageuka kuwa wito mkubwa wa kumpinga rais bashir na utawala wake.

Siku ya Alhamisi Jeshi lilimtimua na kumzuia kiongozi huyo wa muda mrefu Sudan baada ya kuhudumu kwa miaka 30 madarakani.

Aliyeongoza mapinduzi hayo, waziri wa ulizni Awad Ibn Auf, alitangaza kwamba jeshi litasimamia serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka miwili kitakachofuatwa kwa uchaguzi na akaidhinisha miezi mitatu ya hali ya dharura.Jinsi Bashir alivyoweza kudumu mamlakani

Lakini wandamanji waliapa kusalia mitaani hata baada ya hatua hiyo, wakitaka maguezi na kuidhinishwa kwa serikali ya kiraia mara moja.

Ibn Auf himself alijiuzuliu ziku ya pili , kama alivyojiuzulu mkuu wa usalama anayeogopwa na wengi Jenerali Salah Gosh.

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan baada ya hapo alitajwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito la kijeshi, kuwa kiongozi wa tatu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha siku nyingi.

Lt Gen Abdel Fattah Abdelrahman Burhan
Image captionLuteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan ndiye mkuu mpya wa baraza la mpito la kijeshi Sudan

Katika hotuba kwenye televisheni siku ya Jumamosi, Jenerali Burhan aliapa “kuung’oa utawala”, na kuahidi kuheshimu haki za binaadamu, kusitisha marufuku ya kutotoka nje, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuvunjilia mbali serikali zote za majimbo, kuwashtaki waliowaua waandamanaji na kukabiliana na rushwa.

Lakini muungano wa wataalamu Sudan (SPA), ambao umekuwa ukiongoza maandamano hayo umesema muitikio wa baraza hilo “haukudhihirisha matakwa yoyote ya raia” na ametaka maandamano yaendelee.

Miongoni mwa matakwa yao ni kutaka idara ya ulinzi ifanyiwe mageuzi, “viongozi wafisadi” wakamatwe na kuvunjiliwa mbali makundi ya sungusungu yaliohudumu chini ya rais wa zamani Bashir.

Kiongozi huyo wa zamani hajulikani yuko wpai, lakini viongozi wa mapinduzi hayo wanasem ayumpo mahali salama.

Bashir ameshtakiwa kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binaadamu huko Darfur na mahakama ya kimatiafa ya jinai ICC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents