Uncategorized

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Ranieri, Zidane, Mourinho, Allegri, Isco, Chong, Ramos

Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kurejea Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu. (Goal.com)

Meneja wa zamani wa Chelsea, Leicester na Fulham Claudio Ranieri, mwenye umri wa miaka 67, anakaribia kukamilisha taratibu za kuichukua klabu yake ya zamani Roma, a baada ya upande wa ligi hiyo ya dataja la A kumfuta kazi Eusebio di Francesco. (Sky Sports)

Meneja wa zamani wa Chelsea, Leicester na Fulham Claudio Ranieri

Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, mwenye umri wa miaka 46, ambaye amehusishwa na Chelsea, anasakwa na klabu ya Uhispania na Juventus. (Sun)

Mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Isco
Mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Isco ”amemkasirikia” meneja wake Santiago Solari

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, mwenye umri wa miaka 51, amefichua kuwa mazungumzo kuhusu hatma yake ya siku zijazo yamesitishwa hadi mwishoni mwa msimu . (Mail)

Mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Isco, akiwa na umri wa miaka 26, ”amemkasirikia” meneja wake Santiago Solari na ameelezea nia yake ya kuwasiliana na Manchester City. (Calciomercato, via Manchester Evening News)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumtoa kwa timu nyingine winga wao Mjerumani mwenye umri wa miaka 19 kwa deni -kwa msimu wote ujao . (Sun)

Nahodha wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos alikuwa na malumbano makali na rais wa klabu hiyo Florentino Perez kufuatia upande wa hiyo ya Championi kufungwa dhidi ya Ajax, huku Perez akitishia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 . (Marca)

Meneja wa England Gareth Southgate anasisitiza kuwa hakuna mtizamo hasi dhidi ya wachezaji wanaochezea katika mataifa ya kigeni kama winga Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 18- alivyofanya kwa timu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Talksport)

Meneja wa England Gareth Southgate
Meneja wa England Gareth Southgate anasisitiza kuwa hakuna mtizamo hasi dhidi ya wachezaji wanaochezea katika mataifa ya kigeni

Tottenham wamo katika harakati za kurejea White Hart Lane na Haringey Council huku wakitoa taarifa kwa maafisa wa usalama barabarani wakiwataka wahakikishe usalama wa barabarani kwa ajili ya majaribio ya matukio kuanzia mwishoni mwa juma lijalo . (Mail)

Liverpool na Everton wmekuwa wakihusishwa na mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Sociedad ya Uhispania Diego Llorente, mwenye umri wa miaka 25. (Liverpool Echo)

Wakala wa England wamejipanga kukabiliana na Fifa baada ya taarifa juu ya sheria mpya ambazo zinatoza faini zake moja kwa moja na kwa mchezaji wanayemuwakilisha . (Telegraph)

Liverpool itaangalia namna ya kupata mkopo utakaowasaidia kumchukua mchezaji wa Ligi ya Primia Harry Wilson msimu ujao – lakini kuwasili kwa Brendan Rodgers katika Leicester kunaweza kumaliza matumaini ya Foxes ya kusaini mkataba na winga huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni katika Derby. (goal.com)

Mchezaji wa safu ya kati wa Sevilla Muhispania Pablo Sarabia, mwenye umri wa miaka 26, amekataa kuhamia Chelsea mwezi Januari ambacho ndio kipindi cha mwisho cha wachezaji kuhama. (Mundo Deportivo, via Talksport)

Mchezaji wa Ligi ya Primia -Harry Wilson
Liverpool itaangalia namna ya kupata mkopo utakaowasaidia kumchukua mchezaji wa Ligi ya Primia Harry Wilson msimu ujao

Mmiliki wa klabu ya Lille Gerard Lopez amefichua kwamba itagharibu walau pauni milioni £43m kumtoa winga Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ivory Coast huku pia akikanusha mkuruhgenzi wa michezo wa Louis Campos anafanya mazungumzo na Chelsea. (RMC Sport, via Goal.com)

Mchezaji wa safu ya mashambulizi katika mbwa mwitu(wolves) Leo Bonatini, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anacheza kwa deni katika timu ya Nottingham Forest kwa muda uliosalia wa msimu, anataka kubakia City Ground kwa muhula ujao – Forest wapande daraja wasipande . (Express and Star)

Charlton wamepokea maombi mapya ya thamani ya pauni milioni £30m, kutoka kwaafisa wa zamani wa benki mwenye uzoefu wa kiwango cha juucha soka. (London Evening Standard)

Dele Alli
Dele Alli anasema yuko fiti kuingia tena uwanjani baada yakupona majeraha

Brendan Rodgers amepuuza tetesi kwamba afisa mkuu wa kitengo cha utoaji wa kazi wa Celtic Lee Congerton atajiunga nae katika Leicester.(Leicester Mercury)

Mchezaji wa Tottenham, na Mchezaji wa England wa kimataifa anayecheza katika safu ya kati Dele Alli, mwenye umri wa miaka 22, ana matumaini ya kurejea baada ya kupata majeraha Southampton wikendi hii, baada ya kutoshiriki mchezo kutokana na jeraha la mkono tangu Januari 20. (London Evening Standard)

Mshambuliaji klabu ya Uingereza ya Leicester Jamie Vardy
Mshambuliaji klabu ya Uingereza ya Leicester Jamie Vardy anasema yuko Fiti kukabiliana na Fulham baada ya kushonwa ulimi

Mshambuliaji klabu ya Uingereza ya Leicester Jamie Vardy, mwenye umri wa miaka 32, atakua fiti kwa ajili ya kukabiliana na Fulham Jumamosi hii baada ya kufanyiwa upasuaji wa kushona ulimi wake kufuatia kugongana kwake na na Ben Foster ambapo walishindwa 2-1 katika uwanja wa Watford wikendi iliyopita . (Leicester Mercury)

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya Brighton Inigo Calderon, mwenye umri wa miaka 37, amerejea katika klabu ya nyumbani Alaves, nchini Uhispania kama kocha msaidizi kwenye timu hiyo iliyopo kwenye daraja la B nadi mwishoni mwa msimu. (Argus)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents