AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Tetesi za Soka barani Ulaya Jumanne, Morata, Philippe Coutinho, Barella, Suarez, Dybala, Isco, Cesc Fabregas

Manchester United wameanzisha mazungumzo na Barcelona wakitaka kumsajili mshambuliaji Mbrazil Philippe Coutinho, 26, lakini ndipo waweze kumnasa itabidi wachomoe zaidi ya £100m. (Caught Offside)

Philippe Coutinho

Sevilla wamefanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kumchukua mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 26, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Goal.com)

Uhamisho wa Cesc Fabregas kwenda Monaco unakwamishwa na hali kwamba klabu hiyo ya Ligue 1 bado haijaafikiana na klabu ya Chelsea kuhusu ada ya uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 31. (London Evening Standard)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemshauri Fabregas kuihama klabu hiyo ya Stamford Bridge kwa maslahi ya uchezaji wake. (Talksport)

Cesc Fabregas

Wachezaji wa Manchester United wanataka mkufunzi wao kutoka Norway Ole Gunnar Solskjaer apewe rasmi kazi ya umeneja. (Mirror)

Atletico Madrid wamekataa ofa kutoka kwa Manchester United waliokuwa wanamtaka beki wa Uruguay Diego Godin, 32. (Tutto Mercato Web)

Beki wa Ajax anayechezea timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt, 19, amehimizwa kukataa kuhamia Juventus na badala yake ajiunge na Manchester United. (Manchester Evening News)

Real Madrid wameanza harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Denmark Christian Eriksen, 26, kutoka Tottenham na wanajiandaa kutoa takriban £100m kumnasa. (Independent)

Paulo Dybala

Juventus wanasema wanaweza wakashawishika kumuuza Paulo Dybala, 25, ambaye anatafutwa na Manchester City mwisho wa msimu, lakini mradi tu ada ya uhamisho wa raia huyo wa Argentina iwe zaidi ya £90m. (Tuttosport kupitia Express)

Manchester City, Bayern Munich na Paris St-Germain wote wamewasilisha ofa kumtaka Dybala lakini zikakataliwa. (Tuttosport)

Nico

Borussia Dortmund na Bayern Munich wanatarajiwa kuwasilisha ofa kumtaka mshambuliaji wa RB Leipzig anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Timo Werner, 22, ambaye pia amehusishwa na kuhamia Liverpool. (Bild)

Chelsea wanamnyatia kiungo wa kati wa Cagliari Nicolo Barella ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m, lakini huenda wakakumbana na ushindani kutoka kwa Napoli na Inter Milan ambao pia wanataka saini ya kijana huyo wa miaka 21. Mchezaji huyo hata hivyo anadaiwa kutotaka kuihama klabu hiyo ya Serie A wakati wa dirisha la sasa la uhamisho wa wachezaji. (Goal.com)

Denis Suarez

Arsenal wapo katika nafasi nzuri ya kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Yannick Carrasco. Mchezaji huyo wa miaka 25 aliihama Atletico Madrid na kujiunga na klabu ya Dalian Yifang inayocheza Ligi Kuu ya Uchina Februari mwaka jana. (Mirror)

West Ham wanamnyatia mshambuliaji wa Inter Milan kutoka Brazil Gabriel Barbosa. Mchezaji huyo wa miaka 22 – ambaye alikaa klabu ya Santos ya Brazil kwa mkopo miezi 12 iliyopita – amependekezwa kwa West Ham kwa mkpo hadi mwisho wa msimu. (Mirror)

Isco

Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl amethibitisha kwamba klabu hiyo imepokea ofa kutoka kwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Italia Manolo Gabbiadini, 27. (Daily Echo)

Meneja wa Derby Frank Lampard hajafanikiwa katika juhudi zake za kutaka kumchukua kiungo wa kati mkabaji Ethan Ampadu, 18, kutoka kwa klabu yake ya zamani Chelsea. (Independent)

AC Milan wanamtafuta mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, wakitaka kumtumia kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuan, 31. (La Gazzetta dello Sport)

Tammy Abraham in action for Aston Villa

Marco Silva atawasukuma Everton kununua wachezaji Januari iwapo tu wachezaji ambao amekuwa akiwatafuta kwa muda mrefu watakuwa wanauzwa. (Liverpool Echo)

Meneja wa West Brom Darren Moore anapanga kuzungumza na Wes Hoolahan baadaye wiki hii kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo wa miaka 36 kutoka Jamhuri ya Ireland. (Express and Star)

Kiungo wa kati wa Birmingham Luke Maxwell, 21, anatarajiwa kuhamia Solihull Moors kwa mkataba wa kudumu baada ya kukaa nusu ya kwanza ya msimu huu katika klabu hiyo ya Ligi ya Taifa kwa mkopo. (Birmingham Mail)

Kostas Manolas

Barcelona wamejitolea kwa hali na mali kuhakikisha kwamba hawamuuzi kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez, 25, kwa Arsenal mwezi huu. (Mirror)

Wolves wamekamilisha mpango wa kumchukua Tammy Abraham kutoka kwa klabu yake ya Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 21 anatarajiwa sasa kufanya uamuzi leo Jumatatu kuhusu iwpao atakatisha mkopo wake Aston Villa na kwenda Molineux. (Express and Star)

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu beki wa AS Roma kutoka Ugiriki Kostas Manolas, 27, ambaye ana kifungu cha £32m cha kumfungua kutoka kwenye mkataba wake. (Sun)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba haiwezekani kwa winga raia wa England Phil Foden mwenye miaka 18 kuondoka klabu hiyo kwa mkopo. (Independent)

Arsenal hawatarajiwi kuwasili ofa nyingine kumtaka winga wa AS Roma Cengiz Under ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m baada ya ofa yao ya awali ya £35m ya kumtaka mchezaji huyo wa Uturuki mwenye miaka 21 kukataliwa. (Star)


Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW