Michezo

UEFA: Mo Salah, Mane na Firmino wapeleka kilio Italia

Kwa moto huu wa Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane na wa kuuzima?

Klabu ya soka ya Liverpool usiku wa jana imefanikiwa kuingiz mguu mmoja katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuifunga AS Roma kwa mabao 5-2.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Anfield. Liverpool ilipata mabao yake kupitia kwa Salah ailiyefunga mabao mawili (36 na 45), Mane (56) na Firmino aliyefunga mawili pia (61 na 69).

Wakati huo huo mabao ya AS Roma yalifungwa na Edin Dzeko (81) na Diego Perotti (85) kwa njia ya penalty.

Mchezo mwingine wa hatua hiyo ya nusu fainali unatarajiwa kuchezwa leo (Jumatano) ambao utawakutanisha Bayern Munich dhidi ya Real Madrid kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents