Habari

Waadhimisha siku ya tiba ya Wanyama kwa kutoa chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa, paka

BAADHI ya madaktari ya mifumo wameadhimisha Siku ya Tiba ya Wafanya Duniani kwa kutoa chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na paka katika halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho hayo na utoaji wa chanjo hizo, Daktari Bingwa wa Wanyama Wilaya ya Kilolo, Dk. Julius Mahenge amesema kama jamii inavyofahamu ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni hatari kwani unaweza kuhama kutoka kwa mbwa na Kwenda kwa binadamu.

Amesema ugonjwa huo ukiamia kwa binadamu au kwa Wanyama wengine athari zake ni kubwa ikiwemo vifo, hivyo wanatoa chanjo hizo ili kudhibiti ueneaji wa magonjwa hayo ya Wanyama.

“Mbali na kutoa chanjo nimefanya matibabu ya minyoo kwa mbwa wote walioletwa na wafugaji wa hapa Iringa na kuwafundisha mfumo rafiki wa kufuga mbwa ambao hauhatarishi,” amesema Dk. Mahenge
Naye Daktari mwingine wa Wanyama amesema kuwa wamejipanga kuokoa afya za mifugo na binadamu nchini.

Inaelezwa kuwa siku ya Mifugo Duniani (WVD) ni tukio la kila mwaka ambalo huandaliwa na Chama cha Mifugo Duniani kila mwaka. Ni sherehe ya Jumamosi ya mwisho ya Aprili kila mwaka kutambua juhudi za wataalamu wa mifugo duniani kote.

Siku hiyo inaadhimisha majukumu ambayo wataalamu wa mifugo hufanya kwa jamii, na majukumu waliyokabidhiwa. Mwaka huu, WVD imeadhimishwa tarehe 27 Aprili, 2024.

Duniani kote, WVD ilitungwa baada ya uamuzi uliofanywa na Chama cha Mifugo Duniani (WVA) kwa kushirikiana na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH) mnamo 2000.

Nchini Tanzania, kumekuwa na maadhimisho ya WVD kupitia juhudi zinazofanywa na taasisi mbalimbali zinazosimamia shughuli za mifugo hususan Wizara inayohusika na maendeleo ya mifugo na taasisi zake kama vile Kurugenzi ya Huduma za Mifugo (DVS), Baraza la Mifugo Tanzania (VCT) pamoja na Chuo cha Tiba ya Mifugo na Sayansi ya Tiba (CVMBS) katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA).

Ilikuwa hadi mwaka jana (2023) ambapo TVA iliandaa sherehe rasmi ya WVD nchini iliyoadhimishwa jijini Mwanza.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents