Wabunge waliohama Chadema kujiunga NNCR “Tunachangia mil 1.5 kila mwezi hutakiwi kuuliza, Kuna unyanyasaji wa kijinsia na kingono” – Video

Wabunge Joyce Sokombi na Sussane Masele waliotangaza kuhama CHADEMA na kujiunga na NNCR baada ya Bunge kufikia ukomo wameeleza sababu zilizowafanya kuhama CHADEMA ni pamoja na Chama hicho kutokuheshimu katiba yake, pamoja na kukiukwa kwa haki ya kusikilizwa ambapo wabunge wanne wa CHADEMA walifukuzwa uanachama bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

“Sisi wabunge wa viti maalum kila mwezi tunachangia chama Milioni 1.5, kila mmoja amechanga milioni 62, tuko wabunge 37 hivyo tumechangia jumla ya Bilioni 2.2. hatulalamiki kuchanga kwani ipo Kikatiba, tunachohoji ni kwamba matumizi ya fedha hizi hayajawahi kuwekwa wazi na haturuhusiwi kuhoji popote

Madaraka ndani ya CHADEMA yanahodhiwa na wachache wengi wao wakiwa wanaume na hivyo kuwepo mwanya wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono” Sussane Masele Mbunge Viti Maalum.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW