Uncategorized

Waigizaji wa sauti ya rais Uhuru Kenyatta mbaroni kwa tuhuma za wizi wa mamilioni ya fedha

Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.


Watuhumiwa, Antony Wafula, Gilbert Kirunja, David Lukaya and William Malala wakiwa mahakamani hapo jana Jumatatu ya Februari 25 

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni mwenyekiti wa Sameer Africa, akiigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara, kulingana na polisi.

Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi – mtandao wa habari wa gazeti la Daily Nation news umeelezea kuwa zilikuwa ni shilingi milioni 10 ($100,000; £76,000) huku gazeti la Star likisema pesa hizo zilikuwa ni shilingi milioni 80.

Saba hao walifikishwa mhakamani Jumanne, lakini bado hawajashtakiwa.

Polisi wamesema wanahitaji musa zaidi wa kufanya uchunguzi.

“kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano simu ,” ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation.

Jengo la mahakama

Bwana Merali ni mmoja wa wawekezaji wakubwa nchini Kenya katika sekta mbali mbali ikiwemo teknolojia ya mawasiliano pamoja na makazi.

Mtandao wa The Sameer Group unasema kuwa Bwana Merali pia ni mjumbe wa Baraza la serikali la uboreshaji wa masoko ya nje pamoja na baraza la la uwekezaji.

Polisi iliwakamata washukiwa tarehe 22 na 23 Februari.

Wakati wa operesheni hiyo, polisi walikamata magari aina ya Toyota Land Cruiser, Toyota Mark X , Toyota Axio na Toyota Crown.

Uchunguzi huo unatarajiwa kubaini ikiwa magari hayo yana uhusiano na uhalifu huo.

Bwana Merali na rais Kenyatta bado hawajazungumzia juu ya tukio la kukamatwa kwa watu hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents