Uncategorized

Washindi 15 wajinyakulia zawadi kutoka DStv, jiongeze kwa kulipia kifurushi uingie kwenye droo hii ya “Tia Kitu pata vituz”

DKampuni inayoongoza kwa huduma bora za vinga’muzi nchini, DStv  imetangaza washindi 15 wa  droo ya nne ya Promosheni ya “ Tia Kitu pata vituz” ya wiki nane inayoendelea nchi nzima maarufu kama.


Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akichezesha droo ya kupata washindi wa huku Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua  (kulia) akifuatilia kwa makini. Kushoto ni Benson Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv. Promosheni hiyo ni kwa wateja wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo itaendelea kwa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana

Promosheni hiyo ni ya wazi kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika. “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili.” Alisema Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo wakati wa kufanya droo ya wiki ya nne ya promosheni hiyo.

Akizungumza  baada ya kufahamishwa juu ya ushindi wake huo Bw. Issa Mohammed ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Dar es Salaam alisema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi na kuongeza kuwa anaishukuru sana DStv na kuwaasa kuwa waendelea kuwajali wateja wake hivyo hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents