Uncategorized

Waziri wa ulinzi wa Sudan, Awadh Ibn Auf aapishwa rais wa mpito

Waziri wa ulinzi wa Sudan Awadh Ibn Auf ameapishwa kuwa rais wa baraza la mpito la kijeshi, ambalo kulingana na jeshi litaongoza kwa kipindi cha miaka miwili ya mpito.

Kituo cha radio kinachomilikiwa na serikali kimearifu kuwa mkuu wa majeshi Kamal Andel-Marouf ameapishwa kuwa makamu wa rais wa baraza hilo.

Hatua hii imekuja huku waandamanaji wakilalamika kwamba utawala huo wa kijeshi haukumaanisha mabadiliko, na kuahidi kuendelea kuandamana hata baada ya hapo jana kutangazwa kwa sheria inayozuia raia kutembea usiku wa kuanzia saa 4 hadi saa 10 alfajiri.

Rais Omar al Bashir wa Sudan aliyetawala kwa miaka 30, jana Alhamisi alipinduliwa na kukamatwa kufuatia miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga serikali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents