Uncategorized

Yanga yakerwa na kilichoandikwa kwenye gazeti hili ‘Ni uzushi mkubwa, nia yao tusichukue ubingwa msimu huu’

Klabu ya Yanga imeonyesha kukerwa na kitendo cha gazeti la michezo la Championi kuandika maelezo yaliyo husu wachezaji wake kumpinga Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kufuatia kumvua kitambaa cha unahodha beki wake Kelvin Yondani na kudai kuwa habari hiyo inalenga kuwavuruga na kuvunja umoja na ushirikiano kwenye timu hiyo.

Mabingwa hao wazamani wa ligi kuu soka Tanzania Bara wametoa taarifa hizo kupitia kurasa zake za kijamii za Instagram na Facebook.

”KILICHOANDIKWA NA GAZETIHILI NI UZUSHI MKUBWA WANA YANGA WOTE TUUPUUZE, TUNAFAHAMU NIA WALIYONAYO,WAMELENGA KUTUVURUGA HASA KWENYE WAKATI HUU AMBAO UMOJA NA USHIRIKIANO NIMKUBWA KWENYE TIMU YETU…!
HUU NI UZUSHI ULIOLENGA KUKWAMISHA JUHUDI NA MALENGO YAKUTWAA UBINGWA MSIMU.” Imeandika Yanga kupitia kurasa zake za kijamii.

Hapo jana Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongo Mwinyi Zahera alisema kuwa ameamua kumvua unahodha beki wake Kelvin Yondan ‘Vidic’ kufuatia kuwa na vitendo vya utovu wa nidhamu baada ya kushindwa kufika mazoezini pasipo kutoa taarifa na hivyo kuamua kumkabidhi kitambaa hicho Ibrahim Ajibu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents