Uncategorized

Zaidi ya watu 200 wauawa katika shambulio la Makanisa Sri Lanka

Watu 207 wameuawa na wengine 450 kujeruhiwa katika msururu wa mashambulio ya mabomu dhidi ya makanisa na hoteli nchini Sri Lanka.

Milipuko minane imeripotiwa katika mashambulio dhidi ya makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka.

Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zililengwa katika mashambulia hayo.K

Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.

Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo.

Kumekua na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka masariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

Tunafahamu nini kufikia sasa?

Amri ya kutotoka nje imewekwa kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbilia asubuhi kwa saa za Sri Lanka (12:30-00:30 GMT).

Watu saba wamekamatwa kufikia sasa.

Bomu lilipuka wakati vikosi maalum lilipukua likifanya msako katika nyumba moja karibu mjini Colombo
Image captionBomu lilipuka wakati vikosi maalum vikifanya msako katika nyumba moja karibu na mji wa Colombo

Serikali pia imetangaza kuwa itadhibiti matumizi ya mitandao yote ya kijamii kwa mda.

Kanisa la St Sebastian mjini Negombo limeharibiwa vibaya na milipuko hiyo.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha paa la jengo la kanisa lililoharibiwa vibaya huku damu ikiwa imetapakaa ndani ya kanisa.

Karibu watu 67 wameripotiwa kufariki ndani ya kanisa hilo.M

Pia kumeripotiwa idadi kubwa ya watu waliyojeruhiwa katika kanisa la St Anthony mjini Kochchikade, ambao ni moja ya wilaya ya Colombo.

Raia tisa wa mataifa ya kigeni ni miongoni mwa watu waliouawa mjini Colombo, kwa mujibu wa vianzo vya hospitali vilivyozungumza na BBC.

Vyanzo sawia na hivyo mjini Batticaloa vimesema kuwa karibu watu 27 wamefariki mjini humo.

Afisa wa hoteli ya Cinnamon Grand, karibu na makao rasmi ya waziri mkuu wa nchi hiyo,ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mtu mmoja alifariki kutokana na mlipuko huo.

Makasisi wa kanisa la St Anthony, Kochchikade
Image captionKanisa la St Anthony Shrine mjini Kochchikade, ni moja ya makanisa yalioshambuliwa

Ni kinanani walioathiriwa?

Wengi ya waliofariki dunia wanadhaniwa kuwa raia wa Sri Lanka, ambao wa walikuwa wanashiriki ibada ya Jumapili ya Pasaka.

Raia wa kigeni waliothibitishwa kufariki ni Waingereza watano – wawili kati yao wana uraia wa Marekani pia.

Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi Stef Blok katika taarifa yake amethibitisha kifo cha raia mmoja wa nchi hiyo..

WRaia wawili wa Uturuki pia wameripotiwa kuuawa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu.

Waathiriwa

Maafisa wanasema nini?

Rais Maithripala Sirisena ametoa tarifa ya kuwaomba wananchi kuwa watulivu na kuwasaidia maafisa wake katika uchunguzi.

Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe ambaye anaongoza mkutano wa dharura. Amesema: “Nalaani vikali shambuliowatu wetu leo. Natoa wito kwa Wa Sri Lanka wote kuungana wakati huu mgumu.

Katika mtandao wake wa Twitter, Waziri wa Fedha Mangala Samaraweera aliandika mashambulio haya yamepangwa na kutekelezwa ili “Kuua watu, kusababisha taharuki na kugonganisha watuw” na yamesababisha vifo vya “watu wengi wasiokua na hatia”.

Waziri mwingine , Harsha de Silva, amesema mashambulio hayo ni ya kuogofa “Nimeona hali ya kusikitisha ” katika kanisa la St Anthony Shrine mjini Kochchikade, ana kuongeza kuwa ameona ” vipande vya miili ya watu iliyotapakaa kila sehemu”.

Uharibifu

Sri Lanka ina idadi ya wakristo karibu milioni 1.5 ambayo karibu 7% ya watu nchini humo kwa mujibu wa sensa ya mwa 2012.

Dini ya Kibudha inatajwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waumini ambao wanakadiriwa kuwa 70.2% ya watu wote nchini kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni.

Ni dini ambayo pia imepewa nafasi kubwa katika katika katiba ya nchi hiyo ikilinganishwa na dini zingine..

Wahindu na Waislamu wanakadiria 12.6% na 9.7% ya idadi ya watu nchini humo.

uharibifu

Historia ya Sri Lanka

Tangu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kukomeshwa 2009, kumeripotiwa ghasia kw amiaka kadhaa nchini Sri Lanka.

Waumini wa kibudha wamekua wakishambulia misikiti na mali inayomilikiwa na waumini wa dini ya Kiislam.

Hali ambayo ilipelekea kutangazwa kwa hali ya hatari mwezi machi mwaka 2018.F

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalimalizika baada ya wapiganaji wa kundi la Tamil Tigers kushindwa.

Kundi hilo lilipigania uhuru wa jamii ya Tamil walio wachache kwa miaka 26.

Mapigano hayo yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu kati ya 70,000 na 80,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents