Bongo Movie

Rose Ndauka atoka na sinema ya ‘Love Me or Love Me Not’


Msanii wa tasnia ya Filamu Bongo, Rose Ndauka anatarajia kuja na muvi yake ya kwanza kabisa ambayo ameifanya na kampuni yake binafsi inayoitwa Ndauka Entertainment ambayo ndio imesimamia mpango mzima wa utayarishaji na utengenezaji wa muvi hiyo.

Akizungumza na Bongo5 Rose Ndauka alisema muvi hiyo inaitwa “Love Me” na kwamba maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni muvi hiyo kuingia sokoni.

Akiendelea alisema “muvi yangu inatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi mwezi wa sita ambapo itatoka chini ya usimamizi na usambazaji wa kampuni ya Pili Pili Entertainment. Rose aliwataja wasanii wengine walioshiriki katika Muvi hiyo kuwa ni pamoja na Irene Paul na Michael Rodriguez”.

Kuhusu ni wapi muvi hiyo imeshutiwa msanii huyo amesema Muvi yote imefanyika ndani ya Jiji la Dar-Es-Salaam. Amewaomba mashabiki kumpa sapoti pindi Muvi hiyo itakapotoka na kuwaambia kuwa wasubirie makubwa toka Ndauka Entertainment.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents