BurudaniVideos

50 Cent aomba radhi kwa kumdhihaki mlemavu wa akili akidhani teja

50 Cent ameliibua tena. Hivi karibuni alipost video aliyojirekodi akiwa airport kumtania mfanyakazi wa hapo aliyeonekana kama amelewa wakati ni mlemavu wa akili.

https://www.youtube.com/watch?v=d0N8iUkJWkg

Hali ilibadilika baada ya watu wanaomfahamu mtu huyo kumweleza 50 kuwa hayupo kama anavyofikiria bali ni mgonjwa wa akili na hivyo kuifuta post hiyo, japo alikuwa ameshachelewa.

50 aliandika barua kumuomba msamaha kijana huyo aitwaye Andrew Farrell.

0504-50cent-letter-rip-1

Na sasa familia yake imemtaka 50 atoe dola 10,000 kwa taasisi ya Autism Speaks. Mchango huo ni mdogo zaidi ukilinganisha na dola milioni 1 ambazo baba wa kambo wa Andrew alitaka walipwe.

Inadaiwa kuwa baada ya familia ya kijana huyo kupokea barua ya 50 akiomba radhi radhi, imemsamehe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents