Burudani

Hii ndio sababu halisi ya kwanini Big Sean na Ariana Grande wameachana!

Wawakilishi wa mastaa wa muziki wa Marekani, Big Sean na Ariana Grande waliutaja ubusy kuwa ndio sababu za wawili hao kuachana lakini mtandao wa TMZ umeigundua sababu halisi!

big-sean

Vyanzo vilivyo karibu na Ariana Grande vimedai kuwa Big Sean hakuwa akimchukulia mrembo huyo kwa heshima anayostahili na aliandika mashairi yaliyomdhalilisha kwenye wimbo wake Stay Down.

Kwenye wimbo huo Big Sean anarap: I ain’t even gonna lie, I got a million dollar chick, With a billion dollar p****y, Every time I c*m, I swear to God I feel like I be rich.”

Vyanzo vimedai kuwa bibi yake na Ariana alimfuata na kumuuliza kuhusu mashairi hayo aliyohisi yanamdhalilisha mjukuu wake. Hata hivyo Sean anadai kuwa Ariana alimfanya alipe bili zote na alikuwa na matumizi ya kifahari.

Lakini vyanzo vilivyo karibu na Ariana vinasema ni yeye ndiye alikuwa akilipa mara nyingi ikiwemo fedha za mapumziko na gharama za ndege binafsi.

Katika hatua nyingine, Big Sean anadai kuwa kitendo cha Ariana Grande kushikwa makalio jukwaani na Justin Bieber kilifanywa makusudi kumuumiza.

Vyanzo vinasema kuwa Sean anadai ni yeye ndiye aliyemwacha mrembo huyo kwa madai kuwa Ariana ana mambo ya kitoto. Vinasema mfarakano kwenye uhusiano wao ulianza February alipofanya show ya House of Blues na mastaa kibao wakiwemo Kanye, Bieber, JLo, Chris Brown, Jay Z, A$AP Rocky, Tyga, Kylie na Kendall isipokuwa Ariana.

Inasemekana Ariana hakwenda sababu alikuwa akijiandaa na show ya Grammy siku iliyofuata, kitu ambacho Sean hakukipenda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents