Burudani

Wasanii wa Tanzania tunashindwa kutumia nafasi zetu vizuri – Dude

Muigizaji wa vipindi va TV na filamu, Dude amewakumbusha wasanii wenzake kutumia vyema nafasi na vipaji walivyopewa kwa mambo yenye faida zaidi.

11282038_467579806732441_1590049500_n

Dude alifunguka kwa urefu kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Ili ufanikiwe kwenye maisha ni lazma ujitume, ujiepushe na uvivu,ujinga,majungu na fitna, hata km ni tamaa iwe ni ya mafanikio ya jasho lako mwenyewe, watanzania wengi walipata bahati ya kupata fursa adimu kutoka kwa Mungu, iwe vipaji au nafasi muhimu, lkn kwa maajabu wameshindwa kuzitumia, aidha kwa kujiona wao ni bora kuliko wenzao au wao wana akili sana au wao ni watu muhimu sana.

Mfano mzuri wasanii, Mungu alitupa nafasi adimu, lkn tunayoyafanya hayaendani na tunu tuliyopewa na Mungu, kitendo cha kupewa kipaji cha kuwaburudisha watu na kuwaelimisha au kuwaondolea msongo wa mawazo nk hiyo ni baraka kutoka kwa Mungu, lkn kinyume chake tumekuwa tukifanya vitu tofauti na fani zetu, si wamoja, hatupendani,tunafitiniana,tunadharauliana, tunasemana, tunagawanyana, tunavurugana,tunazushiana uongo, tunazibiana nafasi nk.

Lakini tungeacha yote hayo pengine tungekuwa wengine kabisa, labda tungekuwa na maisha mazuri sana yenye kumpendeza Mungu kutokana na upendeleo tuliopewa na Mungu, nashuhudia mengi ndani ya fani yangu ambayo kwa kweli hayana maana kabisa, roho inauma kuona hatuna faida ile inayostahili kutokana na huo ujinga tunaofanya, hatuelewani na wala hatutaki kueleweshana labda kwa kuwa wengi tunaogopana, lkn hali hii mpaka lini hasa!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents