Burudani

Unataka kwenda international? Ben Pol aeleza pressure iliyopo kufanikisha hilo (Video)

Hamasa kubwa ya muziki nchini imekuja na matokeo chanya na hasi na kwa wasanii wengi, changamoto ndio neno linalotawala zaidi.

Tumetaka kujua kutoka kwa Ben Pol nini hasa kinachowatokea wasanii wengine wanapoona wenzao wanafanya mambo makubwa ikiwemo kutengeneza video za gharama kubwa.

“Kiukweli amsha amsha za sasa hivi kwenye muziki zinataleta matokeo mawili kwa msanii ambaye yupo,” anasema Ben.

“Moja naamini wapo watu watakaochoka. Kuchoka kwa maana iko hivyo kwamba unatakiwa utoe hela nyingi ufanye video nzuri iweze kukidhi viwango vya ushindani na vile vile wewe uweze kujipanga vizuri, kujiuza vizuri kwa maana kila kitu chako unavyoonekana, mambo ya photoshoot nzuri, unavyojipresent, collabo unazofanya, kuna collabo zingine inabidi ulipie hela nyingi,” ameongeza.

“Kwahiyo ninachoona ni kwamba kuna watu wataona hizi amsha amsha zimewapita sana, zimeenda mbali sana kwahiyo zitakuwa zinawachosha watu wengine. Lakini kuna wengine akina sisi tutaendelea kusema kwamba siku moja kitaeleweka, tutajaribu kutumia fursa zinazotokea mpaka zitakuja kuwa kitu kikubwa, haijalishi itachukua muda gani.”

“Naamini pia kuna wasanii wenzangu wana mtazamo kama huo kwamba sasa hivi umefika muda wa kujinyima, kujinyima chakula kizuri, kufanya kazi nzuri, kama ni video nzuri, kuisambaza, kuwa na watu wengi timu kubwa inayokusaidia kupush vitu vyako, kukuongoza wewe mentally, kisanaa,” amesema Ben Pol.

Hitmaker huyo wa Sophia amesema ili kufanikiwa kufika mbali asilimia kubwa ya kinachohitajika ni fedha.

“Kwa mfano labda naweza kusema ni asilimia 95 ya watu waliotoboa hizo amsha amsha wametumia hela nyingi, asilimia 5 utakutana na watu ambao wametumia usmart, kudeal na watu sahihi na kutumia zile fursa ndogo ndogo zinazotokea,” amesisitiza.

“Ukitaka kuwa kwenye watu wengi, uaandae tu bajeti nzuri, upige video nzuri angalau hata video ya milioni 15. Lakini ukishindwa hiyo basi deal na watu sahihi angalau hata hicho kidogo unachokipata kiwe kipo kwa ufasaha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents