Bongo Movie
Tin White na Ringo waachia filamu mpya ‘Komando Kipensi’
Wachekeshaji Tin White pamoja na Ringo wameachia filamu yao mpya iitwayo ‘Kombando Kipensi’.
Wawili hao ambao mara nyingi wamekuwa wakiigiza pamoja, wamesema filamu hiyo itakuwa namapigano ndani yake.
“Hii ni filamu ya kuchekesha lakini ndani yake kuna ngumi na mapanga, ni filamu kali sana na leo imeingia sokoni kwa hiyo naweza kusema kila mmoja akanunue nakala yake anaone,” Tin White aliimbia Bongo5.
Kwa sasa wawili hao wanafanya vizuri na show yao na Mahoka ambayo inarushwa katika runinga ya Azam TV.