BurudaniVideos

Vanessa Mdee aeleza mchakato anaopitia katika kuigiza kwenye tamthilia ya MTV Sugar

Vanessa Mdee kwa sasa si muimbaji tu, ameingia kwenye maisha mapya ya uigizaji kwa kishindo.

Mwaka jana alichaguliwa kujiunga kwenye cast ya tamthilia ya MTV Suger.

Staa huyo ameiambia Bongo5 kuwa tayari wameanza kushoot na huenda Afrika Kusini kila baada ya wiki mbili. Amesema katika maandalizi yake, kila muigizaji hupewa script nzima miezi kabla ya kushoot na baadaye hukutana na kuanza kufanya mazoezi na waigizaji wenzake.

Anadai kuwa hulazimika kushika kila kilichoandikwa kwenye script, bila kupunguza ama kuongeza kitu. “Hauongezi wala kupunguza neno lolote na ukiona kama neno haliendani na wewe au huwezi kulikumbuka unaweza kudiscuss na script writers wako on set all the time na kama kuna uwezekano wa kubadilisha wanabadilisha lakini kama haiwezi hakuna,” amesema Vanessa.

Vee amesema kabla ya kuanza kuigiza alikuwa akiogopa sana na sasa baada ya kuona kinachofanyika anawaheshimu zaidi waigizaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents