Burudani

Barnaba: Albamu yangu itakuwa na nyimbo 10 moja ya dini

Barnaba amefunguka kuwa albamu yake mpya itakuwa na nyimbo moja ya dini.

Muimbaji huyo ambaye tangu mapema mwaka jana aliahidi kuachia albamu mwaka huu, amekiambia kipindi cha E News cha EATV kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo kumi moja wapo ikiwa ni wimbo huo wa dini.

“Nina mpango wa kutoa albamu tarehe nane mwenzi wa nane yenye jumla ya nyimbo kumi. Kati ya hizo nyimbo kumi, Lover Boy itakuwa ndani na nyimbo moja itakuwa ya dini na nyimbo nyingine itakuwa bonus ya mashabiki zangu,” amesema Barnaba.

Barnaba ameongeza kuwa albamu hiyo ameipa jina la ‘Lover Boy’ ambalo linatokana na wimbo wake aliouachia miezi mitano iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents