Michezo

Man City kukutana na rungu la FA

Timu ya Manchester City, imeshitakiwa na chama cha soka cha nchini Uingereza FA, kwa kushindwa kuwathibiti wachezaji wake waliomzonga mwamuzi Michael Oliver, katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Man city, wanaweza pigwa faini kwa kosa la hilo la wachezaji wake kwa tukio hilo lilitokea baada ya mwamuzi kuipa Liverpoool, penati.

Oliver alitoa adhabu ya penati baada ya kuona Gary Clichy, amemfanyia madhambi Roberto Frimino, katika eneo la hatari, na penati hiyo ikapigwa na James Milner aliyeukwamisha wavuni.

City wanatakiwa mpaka siku ya Alhamis kuwa wamepeleka utetezi wao kwa chama hicho cha soka cha Uingereza.

Mwamuzi Oliver alipatwa na kadhia kama hiyo ya kuzongwa na wachezaji wa Manchester united wiki iliyopita baada ya kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Ander Herrera katika mchezo wa kombe la FA kati ya Man United na Chelsea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents