BurudaniUncategorized

Nimemfukuza Young Dee sababu ya dawa za kulevya – Max Rioba

Aliyekuwa meneja wa Young Dee kupitia label ya MDB, Max Rioba amekanusha taarifa aliyoitoa rapa huyo kwamba aliondoka kwenye label hiyo baada ya bosi wake huyo kutembea na demu wake aitwae Tunda.

Young Dee akiwa na bosi wake wa zamani, Max Rioba

Max amedai alimfukuza Young Dee baada ya kurudia matumizi ya dawa za kulevya pamoja kukosa nidhamu ya kazi.

“Mimi sikuwahi kumfukuza huyo mtoto kwaajili ya Tunda,” Max alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM. “Nimemfukuza sababu ya matumizi yake ya dawa za kulevya na utovu ya nidhamu na ujinga ujinga wake. Kwani mara ngapi Tunda amekuwa na Dee tukiwa naye hapa, yeye Dee kasema ni moja kati ya sababu za kuondoka hapa, sio kweli sina chochote na huyo mtoto,”

Aliongeza, “Nachojua ni kwamba ana wakati mgumu sana kwenye game, industry imebadilika, kuna watoto wamekuja wanafanya vizuri, ndio maana anaendelea kusema Dimaond hawezi kushuka kwa sababu anajijua anachofanya, Dee hana heshima na nidhamu kwenye kazi hana,”

Rapa huyo hivi karibuni aliambia Bongo5 kuwa aliachana na label hiyo baada ya kushindwa kukubaliana baadhi ya mambo.

“Nikianza na watu ambao nilikuwa nikifanya nao kazi ni watu ambao nilikuwa nafanya nao kazi kama familia. So lilivyokuja suala la kifamilia kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa ndipo ikaoneka kila mtu aanze kufanya kazi mwenyewe bila kumtegemea mtu mwingine,” alisema Young Dee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents