Habari

CCM wahofia kuchukua fomu Kibiti

Wakati hali ya wasiwasi ikizidi kushamiri kwa wakazi wa wilaya za Kibiti na Rufiji juu ya usalama wa maisha yao kutokana na kuendelea kwa matukio ya mauaji, hofu hiyo bado imetanda miongoni mwa wanachama wa CCM wanaohofia kuchukua fomu za kuwania uongozi ngazi ya matawi na shina.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu , Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho katika wilaya hizo, Mussa Mnyeresa amesema sababu za wanachama kususa kuchukua fomu hizo hasa ngazi za tawi, shina na nafasi nyingine ni mfululizo wa matukio ya mauaji yanayoendelea katika wilaya hizi.

Amesema katika wilaya ya Kibiti, kata za Mjawa, Ruaruke na Mchukwi yanaongoza kwa wanachama wa chama hicho kutochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Aidha amesema katika wilaya ya Rufiji uchukuaji fomu za nafasi za uongozi Tarafa ya Ikwiriri yenye Kata tatu za Umwe, Mgomba na Ikwiriri napo zoezi la uchukuaji fomu wa nafasi hizo si la kuridhisha.

Mnyeresa amesema hadi sasa kasi ya uchukuaji fomu hizo katika kata hizo bado ipo chini huku viongozi wa chama hicho wakiendelea kuwahamasisha wanachama wa chama hicho wachukue fomu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents