Habari
Rais Magufuli apokea hati za utambulisho wa mabalozi watano
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli leo jumanne tarehe 01 Agosti 2017 amepokea hati za utambulisho wa mabalozi watano kutoka katika nchi walizotumwa kuja kuziwakilisha nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao kwa Rais Magufuli ni Nguyen Kim Doahu Balozi wa Vietnam, Prof Ratlan Pardede Balozi wa Indonesia, Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solenski Balozi wa Vatican, Dkt Detlef Wachter Balozi wa Ujerumani na Balozi Richard Tumisiime Kabonero kutoka Uganda.
Pitia Taarifa kamili kutoka Ikulu