Michezo
Yanga kuiwekea kambi Simba visiwani Zanzibar
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara klabu ya Dar es salaam Young Afrika inatarajia kufunga safari na kwenda Kisiwani Pemba Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kwa ajili ya maandalizi ya wiki moja kujipanga kumkabili Mnyama Simba katika mchezo wa Ngao ya jamii unaotarajiwa kuchezwa Agosti 23 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka Jijini Dar es Salaam mara baada ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi na kisha kuweka kambi Zanzibar ambapo watapata fursa ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki wakiwa visiwani humo.
Wachezaji wa Kikosi cha Dar es salaam Young Africans
By Hamza Fumo