Burudani

Mrisho Mpoto atua China kwenye Tamasha la Utalii Duniani (Video)

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewasili nchini China Jumatano hii kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Tamasha la Utalii Duaniani.

Mpoto akiwa nchini China

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kitendawili’, aliondoka nchini Tanzania siku ya Jumatatu akiwa ameambatana na kikundi chache cha ngoma kikiwa na jumla ya watu sita pamoja na yeye mwenyewe.

Akiongea na mwandishi wetu akiwa nchini humo baada ya kuwasili katika eneo ambalo litafanyika tamasha hilo, Mpoto amesema Alhamisi hii wataanza kufanya maonyesha hayo katika tamasho hilo ambalo linayakutanisha mataifa mbalimbali duniani.

“Kama nilivyowaambia watanzania wakati naondoka Tanzania, tumekuja China kwaajili ya watanzania, tumekuja kuwawakilisha wao, tunatangaza utalii wa ndani, lugha zetu za makabila zaidi ya 120, lugha yetu hadhimu ya Kiswahili, mbuga zetu za wanyama kwahiyo sisi tutawaambia Tanzania ni nchi ambayo ina kila kitu kama ukiamua kuitembelea,” alisema Mpoto.

Aliongeza,“Tumejiandaa vizuri kufanya kile kitu tulichokipanga, watanzania wananijua mimi ni mtu gani kwenye hizo anga, Kiswahili ni lugha yangu kwahiyo naweza kusema tumejipanga kuuonyesha ulimwengu tuna kitu gani ambacho tumewaletea na bila shaka kila ambaye amekuja katika eneo hili atondoka na meseji ya Tanzania ni sehemu sahihi ya kuitembelea,”

Pia amewataka watanzania kuwaunga mkono wasanii ambao wanafanya jitihada mbalimbali za kuitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za utalii kwa kuwa utalii ni moja kati vyanzo vizuri vya mapato nchini.

“Uwepo wangu mimi hapa sio kwaajili ya familia yangu, hiki ninachokifanya hapa ni kwaajili ya watanzania, yule mtalii ambaye atakuja Tanzania baada ya kusikia meseji yangu ile pesa anayolipa kwaajili ya kutalii ndio ile ambayo inajenga hospitali na kununua dawa. Kwahiyo mimi ningewataka watanzania kuwa wazalendo kwenye mambo ya msingi ambayo bila shaka yanaleta tija kwaajili ya watanzania wote,” alisema Mpoto.

Muimbaji huyo amesema kila mtanzania anaweza kuitangaza nchini yake kwa mazuri hivyo wamewaka watanzania kuwa wazalendo na kudumisha amani iliyopo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents