Burudani

ZaiiD, P The Mc hawana noma na Rostam (Roma & Stamina)

Msanii wa muziki Bongo, ZaiiD amesema ishu ya ngoma yao ‘Miyeyusho’ kufanana idea na ngoma ya Roma na Stamina (Rostam) ‘Hivi Ama Vile’ ni kitu walishakaa na kuzungumza na kuachana nacho.

Miyeyusho ni ngoma ya ZaiiD na P The Mc ambayo inayopatika katika albamu yao itwayo Mwenge Kiwalani iliyotoka mwaka 2014 lakini wimbo wa Rostam August mwaka huu ulionekana kufanana idea na ngoma hiyo.

“Binafsi niongee ukweli ile ngoma yao na yetu ni the same idea, tuna ufanano wa asilimia nyingi, kwa hiyo tulivyosikia tukawa kwenye msahangao ila sisi hatuna noma kwenye kugongana mawazo ni kawaida kwenye muziki,”  ZaiiD ameiambia Bongo5.

“Lakini pia kama tumewasukuma wafanye walichofanya ilikuwa tu kutuambia, kwa hiyo walivyoongea walikuwa na idea hiyo muda mrefu mimi nikaona poa, that hip hop. Nilichati kidogo na Stamina lakni haikuwa kubwa kihivyo, wao waliniambia walikuwa na wazo hilo muda mrefu,” ameongeza.

ZaiiD na P The Mc ambao wanaunda kundi la SSK pamoja na Wakazi na Cjamoker leo wameachia ngoma mpya baada ya kufanya vizuri na ngoma ‘Habari ya Leo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents