Mtibwa Sugar yamnasa kinda aliyecheza michuano ya Gabon
Klabu ya Mtibwa Sugar wamefanikisha kuongeza kandarasi ya Nickson Clement Kibabage kuendelea kutumikia kikosi hicho cha wana tam tam.
Mkataba wa beki huyo wa pembeni ulikuwa unaelekea mwishoni na viongozi wa wana tam tam wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa klabu Jamal Bayser wamefikia makubaliano ya kumuongeza Kibabage kandarasi ya miaka miwili kabla ya mkataba wa awali kumalizika.
Kibabage amesaini kandarasi ya kuendelea kutumikia kikosi katika ofisi ndogo zilizopo jijini Dar es laam chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Jamal Bayser
Nickson Kibabage anayemudu kucheza beki wa pembeni na kiungo mshambuliaji amekuwa katika kiwango bora msimu uliomalizika katika mashindano ya vijana pia katika ngazi ya timu ya taifa ikiwemo kuwakilisha taifa katika mashindano ya CAF nchini Gabon.
Kibabage amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar kupitia cha kukuza vipaji cha Mtibwa Sugar Academy (under 20) na kabla ya hapo alikuwa anachezea Moro Kids.