Michezo

Tshitshimbi awapiku Buswita na Okwi tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari

Shirikisho la soka nchini (TFF), limemtangaza kiungo wa klabu ya Yanga raia wa DR Congo, Papy Kabamba  Tshitshimbi kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Tshitshimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kutupia mabao matatu na kukisaidia kikosi chake cha Yanga kuibuka na alama 12.

Katika kinyang’anyiro hicho Tshitshimbi ameshindana na Pius Buswita wa Yanga SC na Emmanuel Okwi wa Simba SC.

Kawaida mshindi wa tuzo hiyo huzawadiwa kitita cha milioni moja pamoja na king’amuzi cha Azam TV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents