Michezo

Sababu hizi za kisiasa zamzuia Mkhitaryan kwenda kuitumikia Arsenal michuano ya Europa nchini Azerbaijan.

Sababu hizi za kisiasa zamzuia Mkhitaryan kwenda kuitumikia Arsenal michuano ya Europa nchini Azerbaijan.

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hataweza kuwachezea katika mechi yaligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, dhidi ya klabu ya Qarabag. Hii ni kutokana na uhasama wa kisiasa ambao umekuwa ukiendelea kati ya taifa lake la Armenia na Azerbaijan.

Mkhitaryan, 29, hakuweza kusafiri pamoja na wachezaji wenzake kwenda mji mkuu wa taifa hilo, Baku, Jumatano kwa ajili ya mechi hiyo ya Alhamisi.

Hakuna uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya Armenia na Azerbaijan kutokana na mzozo wa muda mrefu kuhusu eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.  “Hawezi kusafiri huko,” meneja wa Arsenal Unai Emery alikiri hilo. “Tuko hapa, wachezaji wana mtazamo mwema na wamejiandaa vyema kucheza.”

Gunners watakutana na Qarabag katika mechi ya Kundi E saa mbili kasoro dakika tano saa za Afrika Mashariki. Uefa wameambia BBC kwamba uamuzi wa pamoja ulifanywa na Arsenal na Mkhitaryan kwamba asisafiri kwa sababu za kiusalama.

Alipokuwa anawachezea Borussia Dortmund mwaka 2015, Mkhitaryan hakuweza kusafiri kwa mechi ya Europa League dhidi ya klabu ya ligi kuu ya Azerbaijan ya Gabala kwa sababu ya wasiwasi kuhusu usalama wake.

Kupitia taarifa, Uefa walisema: “Ni kawaida kwa Uefa kutuma barua za kusaidia mashirika, klabu na afisi za kibalozi katika kupata viza kuwawezesha wachezaji kusafiri kwenda nchi nyingine kucheza mechi za mashindano ya Uefa.”

Alipoulizwa kuhusu mzozo kati ya mataifa hayo mawili, Emery alisema: “Kazi yangu ni kandanda. “Naheshimu utamaduni wa kila mtu na naliheshimu kila taifa, lakini siifahamu hali katika kila taifa. Kwangu, hawezi kucheza.

“Kuna heshima kwake na heshima kwako. Tuko hapa tukiwa na fursa ya kucheza vyema.” Fainali ya Europa League 2019 itachezewa mjini Baku.

Alipoulizwa iwapo Mkhitaryan ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Armenia atasafiri Azerbaijan kucheza fainali iwapo Arsenal watafika hatua hiyo, Emery alisema: “Ni safari ndefu sana kwetu kufika huko fainali.

“Ka sasa, tunaangazia maandalizi ya mechi zijazo.”Mkufunzi mkuu wa Qarabag Gurban Gurbanov alidai Arsenal walijaribu “kumuokoa” Mkhitaryan kutoka kwa “shinikizo” za kuchezea Azerbaijan. “Sikutaka siasa ziingilie mchezo lakini hatungefanya jambo lolote zaidi kuhusu suala hilo,” alisema.

“Iwapo Henrikh Mkhitaryan atataka kuja Azerbaijan, haitakuwa mara ya kwanza – wachezaji wengi wa Armenia huja Azerbaijan lakini ni uamuzi wa Arsenal kwamba asije.”Arsenal huenda wana wasiwasi kwamba mbele ya mashabiki 60,000 wa Azerbaijan, Mkhitaryan atakuwa na shinikizo sana na kushindwa kucheza na ndiyo sababu hawakusafiri naye Mkhitaryan.”

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents