Michezo

Baada ya kupachika goli mbili siku ya jumamosi Ronaldo, jana na familia yake walienda Ureno kushuhudia Derby hii kubwa nchini humo

Ikumbukwe katika kila nchi na kila mji kuna timu kubwa ambazo zinawapinzani wao wakubwa katika miji hiyo. mfano nchini Uingereza derby kubwa yaani timu kubwa zinazotoka katika mji mmoja ni Manchester united dhidi ya Manchester City.

Na katika mji wa Madrid derby kubwa ni kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid na mjini Lisbon Derby kubwa ni kati ya Sporting club dhidi ya Benifica zote kutoka Ureno.

Katika mchezo huo Mbabe wa magoli duniani Cristiano Ronaldo na familia yake walisafiri kutoka nchini Italia mpaka Ureno kushuhudia mtanange mkali kati ya timu yake ya zamani Sporting club iliyomkuza dhidi ya Benifica zote zikitoka katika mji huo na katika mtanange huo ulishuhudiwa Sporting akip[oteza dhidi ya Benifica.Benifica wakiwa ugenini waliibuka na ushindi wa jumla ya magoli 4-2.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents