Habari

Rais Magufuli awataka mashabiki wa Simba na Yanga waungane, atoa zawadi nono kwa Taifa Stars na Mwakinyo (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli amewataka mashabiki wa timu za Simba na Yanga waungane na kushangilia pindi timu hizo zinapocheza michezo ya kimataifa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 25, 2019 Ikulu Jijini Dar Es Salaam, kwenye hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Hassan Mwakinyo kwa ushindi walioupata wikiendi iliyopita.

Niwaombe Watanzania hasa mashabiki wa Yanga na Simba, inapocheza Simba katika michezo ya kimataifa basi tuishangilie Simba,pia inapocheza Yanga nayo tuishangilie, inawezekana hivi ndio vinatuchelewesha,” – amesema Rais Magufuli na kumpongeza bondia Mwakinyo.

Nampongeza sana bondia Hassani ambaye nimefuatilia historia yake ameanza kufanya mazoezi kwenye matairi mpaka mikono ikawa na sugu hadi akampiga yule bondia akaanguka chini,”amesemaRais Magufuli .

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewazawadia viwanja wachezaji wa Taifa Stars na bondia Mwakinyo.

Kwa wachezaji hawa walioshinda Taifa Stars pamoja na Hassani Mwakinyo na mwalimu wake ikiwa pamoja na Tenga na Tino, Waziri Mkuu usimamie viwanja Dodoma Makao makuu, kila mmoja apate kiwanja chake cha kujenga nyumba,” amesema Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents